Diamond Platnumz Atajwa Tuzo za MTV EMA

Diamond Platnumz Atajwa Tuzo za MTV EMA

Diamond Platnumz Atajwa Tuzo za MTV EMA

Nyota wa muziki wa Bongo Fleva na Afrika Mashariki, Diamond Platnumz, amepata uteuzi mwingine wa kuwania tuzo zinazotambulika kimataifa, MTV Europe Music Awards (EMA) 2024.

Mwimbaji huyu wa Bongoflavour amechaguliwa katika kipengele cha “Best African Act”, akichuana vikali na wasanii wengine wenye majina makubwa barani Afrika, akiwemo Asake na Ayra Starr kutoka Nigeria, Tyla, Titom & Yuppe, na DBN Gogo kutoka Afrika Kusini.

Diamond Platnumz Atajwa Tuzo za MTV EMA

Hii si mara ya kwanza kwa Diamond kuwania tuzo hizi zinazoenzi wasanii bora duniani. Mwaka 2023, aliibuka mshindi katika kipengele hicho hicho, akiwa msanii pekee kutoka Afrika Mashariki aliyeteuliwa. Ushindi huo ulikuwa wa kihistoria kwake na kwa Tanzania kwa ujumla, ukimshuhudia akipambana na majina makubwa kama Burna Boy na Asake kutoka Nigeria.

Diamond ana historia nzuri linapokuja swala la tuzo za MTV EMA. Mwaka 2015, aliweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza Afrika kushinda tuzo tatu za EMA ndani ya usiku mmoja. Alishinda tuzo ya “Best African Act”, “Best Worldwide Act (Africa/India)”, na “Best African Act” tena mwaka jana, 2023.

Je, Diamond ataweza kuendeleza utawala wake na kushinda tena mwaka huu? Zoezi la upigaji kura limeanza rasmi kupitia tovuti ya mtvema.com. Mashabiki wanaweza kumpigia kura msanii wao kipenzi hadi tarehe 10 Novemba 2024, ambapo tuzo hizo zitatolewa mjini Manchester, Uingereza.

Ushindi wa Diamond katika tuzo hizi utakuwa ni ushindi mkubwa kwa muziki wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, ukionyesha ukuaji na utambuzi wa vipaji vya wasanii wetu kimataifa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Huu Apa Wimbo Mpya wa Nay Wa Mitego Ft Raydiace – Nitasema
  2. Jux na Diamond Watamba na Wimbo Mpya Ololufe – Sikiliza Hapa
  3. Washindi wa Tuzo za MTV VMA 2024
  4. Tyla Ashinda Tuzo ya Video Bora ya Muziki wa Kiafrika VMA 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo