CV ya Miloud Hamdi, Kocha Mpya wa Yanga 2025 | Wasifu wa Kocha Mpya wa Yanga Miloud Hamdi
Muda mfupi baada ya kuachana na kocha Sead Ramovic, Klabu ya Young Africans (Yanga SC) imetangaza rasmi kumpa nafasi Miloud Hamdi, kocha raia wa Algeria na Ufaransa, kama kocha mkuu mpya wa timu hiyo.
Taarifa rasmi iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo imeeleza kuwa Miloud Hamdi ana uzoefu mkubwa wa kufundisha soka barani Ulaya, Asia, na Afrika, na ataungana na kikosi cha Yanga mara moja kuanza majukumu yake mapya.
Kocha Hamdi ameonyesha mafanikio makubwa katika taaluma yake ya ukocha, akiwahi kushinda taji la Ligi Kuu ya Algeria na kufikia fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na klabu ya USM Alger. Ujio wake unaleta matumaini mapya kwa mashabiki wa Yanga, huku wengi wakitarajia mafanikio makubwa kwa klabu hiyo.
TAARIFA KWA UMMA #TimuYaWananchi #DaimaMbeleNyumaMwiko pic.twitter.com/Loe5jc2lGZ
— Young Africans SC (@YoungAfricansSC) February 4, 2025
Wasifu wa Miloud Hamdi
Miloud Hamdi alizaliwa mnamo Juni 1, 1971, na ana uraia wa Algeria na Ufaransa. Uzoefu wake mkubwa wa kufundisha soka unadhihirishwa na kazi alizofanya katika mabara matatu tofauti—Ulaya, Asia, na Afrika. Hamdi amepata diploma ya ukocha kutoka Shirikisho la Soka la Ufaransa, akimiliki leseni ya UEFA A, ambayo ni miongoni mwa viwango vya juu zaidi vya taaluma ya ukocha duniani.
Taarifa | Maelezo |
Jina Kamili | Miloud Hamdi |
Tarehe ya Kuzaliwa | Juni 1, 1971 |
Uraia | Algeria, Ufaransa |
Leseni ya Ukocha | UEFA A Licence |
Lugha | Kiingereza, Kiarabu, Kifaransa, Kiitaliano |
Mfumo Pendwa | 4-2-3-1 |
Mwanzo wa Safari ya Ukocha
Hamdi alianza safari yake ya ukocha mwaka 2004 akiwa na ES Vitrolles ya Ufaransa. Baadaye, alihamia GS Consolat Marseille, ambapo alipata mafanikio makubwa kwa kuiongoza timu hiyo kushinda ubingwa wa Championnat National mwaka 2011/2012. Baada ya hapo, alipata nafasi ya kuinoa Sanremese Calcio ya Italia.
Mafanikio Barani Afrika
Mwaka 2015, Hamdi alielekea barani Afrika ambapo alijiunga na USM Alger ya Algeria. Huko, alipata mafanikio makubwa kwa kuiongoza timu hiyo kushinda taji la Ligi Kuu ya Algeria mwaka 2015/2016 na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huo huo.
Baada ya USM Alger, Hamdi alizifundisha timu mbalimbali barani Afrika, ikiwemo RS Berkane ya Morocco, Al-Salmiya SC ya Kuwait, CS Constantine ya Algeria, JS Kabylie ya Algeria, na Al-Khaldiya FC ya Bahrain.
Uzoefu wa Kazi wa Miloud Hamdi Kocha Mpya wa Yanga 2025
Hamdi ameweza kuhudumu kama kocha katika vilabu mbalimbali kwa mafanikio makubwa. Hapa chini ni orodha ya baadhi ya timu alizozinoa:
- Al-Kalidiya SC (2023-2024) – Kocha Mkuu
- JS Kabylie (2022-2023) – Kocha Mkuu
- CS Constantine (2020-2021) – Kocha Mkuu
- Al-Salmiya SC (2019-2020) – Kocha Mkuu
- USM Alger (2018-2019) – Kocha Mkuu
- RS Berkane (2016-2017) – Kocha Mkuu
- USM Alger (2015-2016) – Kocha Mkuu
- Al Ettifaq (2012-2015) – Kocha Mkuu
- Marseille Consolat (2009-2013) – Kocha Mkuu
- Sanremese (2006-2008) – Kocha Mkuu
Katika kila klabu, Hamdi ameonyesha uwezo wa kuboresha kiwango cha timu na kushirikiana vizuri na wachezaji, hasa katika mashindano ya kimataifa.
Umuhimu wa Ujio wa Hamdi kwa Yanga
Kocha Miloud Hamdi analeta uzoefu wa kipekee na rekodi ya mafanikio ambayo inaweza kusaidia Yanga kufanikisha malengo yake msimu huu. Ujuzi wake wa soka la Afrika, Ulaya, na Asia unatoa nafasi nzuri kwa klabu hiyo kuimarisha ushindani wake katika mashindano ya ndani na ya kimataifa.
Hamdi, ambaye alikuwa kocha wa Singida Black Stars kabla ya kujiunga na Yanga, anachukua jukumu hili jipya akiwa hajafundisha mechi yoyote ya mashindano katika timu hiyo ya zamani. Uteuzi wake umeonyesha dhamira ya Yanga ya kuimarisha benchi la ufundi kwa lengo la kushinda mataji zaidi na kuendelea kuwa klabu bora barani Afrika.
Kwa mashabiki wa Yanga, ujio wa Hamdi unaleta matumaini mapya, hasa kutokana na historia yake ya mafanikio katika ngazi ya juu ya soka. Mashabiki wanatarajia kuona mabadiliko chanya chini ya uongozi wake.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Timu zilizofuzu 32 bora CRDB Bank Federation Cup 2024/2025
- Vinara wa Assist NBC Premier League 2024/2025
- Ratiba ya Mechi za Yanga February 2025
- Kikosi cha Yanga Vs Kagera Sugar Leo 01/02/2025
- Aliekua Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi Atua Al Nasr ya Libya
- Kagera Sugar Yatamba Kuondoa Unyonge KMC Complex Dhidi ya Yanga
- Morocco Aweka Mikakati ya Ushindi dhidi ya Vigogo Ndani ya Kundi C AFCON 2025
- Simba SC Yajiandaa Vikali Kuisambaratisha Tabora United
- Makundi ya Fainali za Mataifa ya Afrika AFCON 2025
- Tanzania Yapangwa Kundi C AFCON 2025
- Kundi la Taifa Stars AFCON 2025
- Kundi la Stars AFCON 2025 Kufahamika Leo
- Ramovic Aelezea Sababu za Ikanga Kukosa Mchezo wa Kombe la Shirikisho
Leave a Reply