CV ya Ahoua Jean Charles Mchezaji Mpya Wa Simba 2024/2025: Klabu ya Simba SC imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Ahoua Jean Charles raia wa Ivory Coast 🇨🇮 kwa mkataba wa miaka miwili. Ahoua kinda fundi wa boli mtoto wa afu mbili mwenye umri wa miaka 22 ametokea Stella Club d’Adjamé ya nchini kwao Ivory Coast huku akiwa ndiye MVP wa msimu wa 2023/2024.
Katika msimu wa 2023/24, Ahoua ameibuka kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu nchini Ivory Coast (MVP) na klabu yake, huku akifunga mabao 12 na kutoa ‘assist’ tisa. Kiungo huyu mshambuliaji anasifika kwa kufunga mabao mengi nje ya box, kuchezesha timu, pamoja na kutengeneza nafasi kwa wenzie.
Mashabiki wengi wa simba wanategemea mambo makubwa kutoka kwa Ahoua kwa kushirikiana na nyota wengine ambao wameshasajiliwa pamoja na wale waliokuwepo kikosini. Kuelekea msimu wa Ligi 2024/25, Klabu ya Simba imekuja na utaratibu mpya kwenye usajili wa kuingiza wachezaji bora wenye uwezo na umri mdogo ili kujenga timu imara ya muda mrefu.
Ahoua anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa baada ya Lameck Lawi, Joshua Mutale, na Steven Mukwala. Usajili huu ni hatua muhimu kwa Simba SC, ikilenga kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya michuano mbalimbali ndani na nje ya nchi. Wapenzi na mashabiki wa Simba SC wana matumaini makubwa kuona mchango wa Ahoua katika kufanikisha malengo ya klabu kwa msimu ujao.
Angalia Hapa: Tetesi za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025
CV ya Ahoua Jean Charles Mchezaji Mpya Wa Simba 2024/2025
Kipengele | Maelezo |
Tarehe ya kuzaliwa/Umri | 10 Februari, 2002 (22) |
Mahali pa kuzaliwa | Zikisso, Cote d’Ivoire |
Urefu | 1.73 m |
Uraia | Cote d’Ivoire |
Nafasi | Kiungo – Kiungo mshambuliaji |
Mguu | wa kulia |
Wakala wa mchezaji | Jamaa |
Klabu ya sasa | Simba SC |
Alijiunga | 3 Julai, 2024 |
Alipotoka | Stella Club d’Adjamé |
Mkataba unaisha | 2026 |
Nafasi kuu | Kiungo mshambuliaji |
Nafasi nyingine | Winga wa kulia na winga wa kushoto |
Habari Zinazo Trend:Â
- Tetesi za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025
- Tetesi za Usajili simba 2024/2025
- Tetesi za Usajili Real Madrid 2024/2025
Safari ya Soka ya Ahoua Jean Charles
Ahoua Jean Charles ameanza safari yake ya soka la kulipwa kwa umahiri mkubwa, akionesha kiwango bora katika klabu mbalimbali nchini Cote d’Ivoire. Huu hapa ni muhtasari wa historia ya uhamisho wake:
Msimu | Tarehe | Klabu Aliyoondoka | Klabu Aliyojiunga |
20/21 | 1 Julai, 2020 | LYS Sassandra | Séwé Sports |
22/23 | 1 Julai, 2022 | Séwé Sports | Stella Club |
Hii Apa Video Ya Baadhi Ya magoli Hatari Alofunga Ahoua Jean Charles
Jean Ahoua mrithi fundi mpya Msimbazi ✨ pic.twitter.com/Jkwe6iNQfA
— SportsArenaTz (@SportsarenatzTz) July 3, 2024
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply