CS Sfaxien vs Simba SC Leo 05/01/2024 Saa Ngapi?
BAADA ya Yanga kumalizana na TP Mazembe ya DR Congo kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika jana, leo ni zamu ya wekundu wa Msimbazi, Simba SC. Timu hiyo maarufu ya Tanzania inakutana na CS Sfaxien kutoka Tunisia kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika (#TotalEnergiesCACC). Mechi hii itapigwa kwenye Uwanja wa Olympique Hammadi Agrebi jijini Tunis. Ushindi wa Simba leo utakuwa hatua muhimu kuelekea kufuzu robo fainali ya michuano hii mikubwa barani Afrika.
Simba SC inakuja kwenye mechi hii ikiwa na pointi sita baada ya michezo mitatu ya Kundi A, hali inayowapa nafasi nzuri ya kuongoza kundi lao endapo wataibuka na ushindi. Kwa upande wa CS Sfaxien, watakuwa wakitumia faida ya uwanja wa nyumbani ili kuwapa mashabiki wao furaha ya ushindi dhidi ya wapinzani wao kutoka Tanzania.
Muda wa Mechi na Mahali
- Mechi: CS Sfaxien vs Simba SC
- Tarehe: 05 Januari 2024
- Muda: Saa 1:00 usiku (kwa saa za Afrika Mashariki)
- Uwanja: Olympique Hammadi Agrebi, Tunis, Tunisia
Umuhimu wa Ushindi kwa Simba SC: Simba SC imekuwa moja ya timu zenye rekodi bora kwenye michuano ya CAF katika miaka ya hivi karibuni. Ushindi leo utaifanya kufikisha pointi tisa, hatua itakayoiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali kwa mara ya sita katika misimu saba ya kushiriki michuano ya CAF.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Msimamo wa Kundi la Yanga Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025
- Kikosi cha Yanga vs Tp Mazembe Leo 04/01/2024
- Yanga Kuwakosa Maxi, Chama na Yao Mechi Dhidi ya TP Mazembe Leo
- Yanga vs Tp Mazembe Leo 04/01/2024 Saa Ngapi?
- Kikosi cha Kilimanjaro Stars VS Zanzibar Heroes leo 03/01/2024
- Viingilio Mechi ya Yanga VS TP Mazembe 04/01/2025
Leave a Reply