CS Constantine vs Simba Leo 08/12/2024 Saa Ngapi?

CS Constantine vs Simba Leo Saa Ngapi

CS Constantine vs Simba Leo 08/12/2024 Saa Ngapi?

Baada ya Yanga SC kushindwa kutamba dhidi ya MC Alger na kukubali kichapo cha goli 2-0 na kushindwa kupeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya CAF, leo Simba SC wanapokea kijiti na kushuka dimbani kuwakabili wenyeji wao CS Constantine katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho CAF. Hapa tumekuletea taarifa kamili kuhusu mchezo huu, ikiwemo uwanja utakaochezewa, muda wa mchezo, na chaneli ya kuutazama mubashara.

Muda na Mahali Mchezo Utakapochezwa

Mchezo wa CS Constantine dhidi ya Simba SC unatarajiwa kuchezwa leo, tarehe 08 Disemba 2024, katika Uwanja wa Mohamed-Hamlaoui, uliopo nchini Algeria. Uwanja huu ni maarufu kwa kuwa wenyeji wa timu ya CS Constantine, moja ya klabu kongwe na zenye mafanikio makubwa katika soka la Algeria. Mchezo utaanza rasmi saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

CS Constantine vs Simba Leo 08/12/2024 Saa Ngapi?

Kwa mashabiki wa soka wa Simba SC na CS Constantine, mechi hii itarushwa mubashara kupitia kisimbuzi cha Azam, kwenye chaneli ya AzamSportHD. Hakikisha unakuwa na kifurushi chenye chaneli hiyo ili usipitwe na matukio yote ya mchezo.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo wa Kundi la Yanga Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025
  2. Yanga Yapasuka Tena Klabu Bingwa, Yachapwa 2-0 na MC Alger
  3. Matokeo ya MC Alger VS Yanga SC Leo 7/12/2024
  4. Kikosi cha Yanga SC vs MC Alger Leo 7/12/2024
  5. Ushindi wa Namungo dhidi ya Tanesco Wampa Mgunda Tumaini
  6. Hizi Apa Mbinu Za Fadlu Za Kuisambaratisha CS Constantine
  7. MC Alger Vs Yanga Leo 07/12/2024 Saa ngapi?
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo