Coastal Union Vs Simba Leo 01/03/2025 Saa Ngapi?
Wanamangushi wa Coastal Union leo wataikaribisha Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Hii ni mechi muhimu kwa timu zote mbili, huku Simba ikisaka alama tatu muhimu kuendelea na mbio za ubingwa, na Coastal Union ikihitaji ushindi ili kujinusuru kutoka katika nafasi za chini za msimamo wa ligi.
Taarifa Muhimu Za Mechi Coastal Union Vs Simba Leo
- Tarehe: 01 Machi 2025
- Uwanja: Sheikh Amri Abeid, Arusha
- Muda: Saa 10:00 jioni
- Matokeo ya mzunguko wa kwanza: Simba 2-2 Coastal Union
- Mchezaji wa kufuatilia Coastal Union: Maabad Maabad (Mabao 5)
- Mchezaji wa kufuatilia Simba: Jean Charles Ahoua (Mabao 10)
- Matokeo ya mechi 5 za mwisho za Coastal: W-1, D-3, L-1
- Matokeo ya mechi 5 za mwisho za Simba: W-3, D-2, L-0
Muktadha wa Mchezo
Simba SC inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na presha kubwa baada ya kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Azam FC katika mechi iliyopita. Matokeo haya yaliifanya Simba kubaki na alama 51, ikiwa nyuma ya vinara Yanga SC waliokuwa na pointi 58 kabla ya mchezo wao wa jana dhidi ya Pamba Jiji. Hivyo, ushindi leo utasaidia Wekundu wa Msimbazi kuendelea kusalia kwenye mbio za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.
Kwa upande wa Coastal Union, mchezo huu ni wa hesabu ngumu. Wagosi wa Kaya wanahitaji pointi tatu ili kujiondoa kwenye presha ya kushuka daraja. Kwa sasa wana alama 24 baada ya mechi 21, na iwapo watapoteza mchezo wa leo, wanaweza kusogezwa chini zaidi na timu zinazowafuatia kwenye msimamo wa ligi.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Mashujaa FC Yathibitisha Kumfuta Kazi Kocha Mohamed Abdallah ‘Baress’
- Arajiga Kuchezesha Mechi ya Kufuzu Kombe La Dunia 2026
- Twiga Stars Yavuka Raundi ya Pili WAFCON Baada ya Sare Dhidi ya Guinea
- Antony Afutiwa Kadi Nyekundu, Sasa Ruksa Kuivaa Madrid
- Matokeo ya Equatorial Guinea vs Twiga Star Leo 26/02/2024
- Man United Wamnyemelea Xavi Kuchukua Mikoba ya Amorim
- Kocha Melis Medo Atua Singida Black Stars Kama Kocha Msaidizi
Leave a Reply