Bayer Leverkusen Imeweka Rekodi ya kushinda Kombe La Bundesliga bila kufungwa

Bayer Leverkusen Imeweka Rekodi ya kushinda Kombe La Bundesliga bila kufungwa

Msimu wa 2023/2024 bila shaka utaandikwa kwa wino wa kukorezwa katika kitabu cha historia cha soka la Ujerumani baada ya mabibingwa wa ligi kuu Ujerumani Bundesliga Bayer Leverkusen kumaliza msimu wakiwa hawajapoteza mchezo wowote. Bayer Leverkusen wamefanya kile ambacho hakuna timu nyingine iliyowahi kukifanya: kushinda taji la ligi kuu ya Ujerumani bila kupoteza mchezo hata mmoja! licha ya mabingwa wa muda wote Bayern munich kutwaa kombe ilo mara nyingi zaidi.

Bayer Leverkusen Imeweka Rekodi ya kushinda Kombe La Bundesliga bila kufungwa

Bayer Leverkusen Imeweka Rekodi ya kushinda Kombe La Bundesliga bila kufungwa

Katika siku ya mwisho ya msimu, Leverkusen walisherekea ushindi wa 2-1 dhidi ya Augsburg mbele ya mashabiki wao wa nyumbani katika dimba la BayArena. Mabao ya Victor Boniface na Robert Andrich yaliihakikishia Leverkusen ushindi huo, huku Augsburg wakipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Mert Komur.

Leverkusen walimaliza msimu wakiwa na pointi 90, wakishinda michezo 28 na kutoka sare mara sita. Hii iliwaweka pointi 17 mbele ya Stuttgart waliomaliza katika nafasi ya pili. Bayern Munich walikuwa wa tatu, Leipzig wa nne na Borussia Dortmund wa tano.

Ushindi huu wa Leverkusen haukuwa tu katika Bundesliga. Timu hii imekuwa kwenye kiwango cha juu kwa muda mrefu, wakicheza michezo 51 mfululizo bila kupoteza katika michuano yote. Hii ni pamoja na kufika fainali ya Europa League, ambapo walilazimishwa sare ya 2-2 na AS Roma, lakini wakafuzu kwa ushindi wa jumla wa 3-2.

Sare dhidi ya Roma ilikuwa ya kihistoria kwa Leverkusen, kwani iliwaweka katika rekodi ya timu ambayo haijapoteza mechi nyingi mfululizo barani Ulaya, wakifikisha michezo 49 bila kupoteza. Hata hivyo, Leverkusen walipoteza fainali ya Europa League dhidi ya Sevilla kwa mikwaju ya penalti.

Nini Kinafuata kwa Leverkusen?

Baada ya kuibuka na ubingwa wa kombe la Bundesliga, Leverkusen sasa wamejihakikishia nafasi ya kushiriki katika Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA msimu ujao. Mashabiki wao wana matumaini makubwa kwamba timu yao itaendelea na moto huu katika michuano ya Ulaya.

Mapendekezo Ya Mhariri:

  1. Zamalek Yashinda Kombe la Shirikisho CAF 2023/2024
  2. Historia Mpya Yaandikwa: Man City Yanyakua Taji la EPL kwa Mara ya 4 Mfululizo
  3. Marefa wa Tanzania waliochaguliwa Kuchezesha Michezo ya Kufuzu Kombe la Dunia
  4. Timu Zilizofuzu UEFA Champions League 2024/2025
  5. Magoli Mawili ya Haaland Yarejesha Man City Kileleni mwa Msimamo wa Ligi
  6. Mvua Yafichua Ubovu wa Old Trafford: Video ya Kuvuja Maji Yatisha Mashabiki
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo