Baraka Majogoro Karibu Kujiunga na Orlando Pirates
Kiungo wa Chippa United, Mtanzania Baraka Majogoro, hayupo kwenye kikosi cha timu hiyo kwa wiki ya tatu sasa, huku ripoti zikieleza kuwa yupo kwenye hatua za mwisho za kujiunga na klabu ya Orlando Pirates inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Majogoro, ambaye alikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Chippa United, amecheza mechi 16 katika msimu wake wa kwanza na msimu huu ameshiriki kwenye michezo minane, akionyesha uwezo mkubwa wa kucheza katika safu ya kiungo wa kati.
Safari ya Majogoro Afrika Kusini
Huu ulikuwa msimu wa pili kwa Majogoro kucheza soka la kulipwa Afrika Kusini. Hapo awali, alikuwa miongoni mwa wachezaji wachache wa Kitanzania waliokuwa wakisakata kandanda katika ligi hiyo, baada ya Gadiel Michael kurejea Tanzania kujiunga na Singida Black Stars na Abdi Banda kutimkia Dodoma Jiji kutoka Baroka FC.
Taarifa kutoka kwa chanzo cha kuaminika zinaeleza kuwa Majogoro ana nafasi kubwa ya kujiunga na Orlando Pirates bila ada ya uhamisho baada ya kuvunjiwa mkataba na Chippa United. Chanzo hicho kilisema:
“Mawasiliano kati ya Majogoro na uongozi wa Orlando Pirates yamekuwa na matumaini makubwa. Mazungumzo yalikwenda vizuri Jumanne iliyopita, na ninachojua ni kwamba atajiunga bure kwa sababu Chippa United imemvunjia mkataba.”
Orlando Pirates Yavutiwa na Majogoro
Kocha wa Orlando Pirates, José Riveiro, ameripotiwa kuidhinisha usajili wa Majogoro na anaonyesha nia kubwa ya kumjumuisha kwenye kikosi chake. Mchezaji huyo anasifika kwa nidhamu kubwa na uwezo wa kucheza kama kiungo mkabaji, nafasi ambayo Riveiro anaamini inaweza kuimarisha timu yake. Hata hivyo, mpaka sasa Majogoro hajazungumza hadharani kuhusu mustakabali wake, na juhudi za kumpata kwa mahojiano hazijazaa matunda.
Majogoro mara ya mwisho alionekana uwanjani Desemba 29, alipocheza kwa dakika 56 dhidi ya Kaizer Chiefs katika mechi ambayo Chippa United ilipoteza kwa bao 1-0. Tangu wakati huo, hajakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo, jambo linaloashiria uwezekano mkubwa wa kuhamia Orlando Pirates.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Hat Trick Dhidi ya Coastal Yampa Mukwala Mzuka Kuelekea Dabi ya Kariakoo
- Matokeo ya Coastal Union vs Simba Leo 01/03/2025
- Kikosi cha Simba vs Coastal Union Leo 01/03/2025
- Coastal Union Vs Simba Leo 01/03/2025 Saa Ngapi?
- Mashujaa FC Yathibitisha Kumfuta Kazi Kocha Mohamed Abdallah ‘Baress’
- Arajiga Kuchezesha Mechi ya Kufuzu Kombe La Dunia 2026
- Twiga Stars Yavuka Raundi ya Pili WAFCON Baada ya Sare Dhidi ya Guinea
- Antony Afutiwa Kadi Nyekundu, Sasa Ruksa Kuivaa Madrid
- Matokeo ya Equatorial Guinea vs Twiga Star Leo 26/02/2024
Leave a Reply