Banda Avunja Mkataba na Baroka FC Baada ya Miezi 3 Tu

Banda Avunja Mkataba na Baroka FC Baada ya Miezi 3 Tu

Banda Avunja Mkataba na Baroka FC Baada ya Miezi 3 Tu

BEKI Mtanzania, Abdi Banda, amevunja mkataba wake na Baroka FC ya Afrika Kusini baada ya miezi mitatu tu tangu ajiunge na klabu hiyo inayoshiriki Ligi ya Championship. Uamuzi huu unakuja baada ya makubaliano ya pande zote mbili, ambapo Banda sasa anatafuta changamoto mpya katika taaluma yake ya soka.

Banda Avunja Mkataba na Baroka FC Baada ya Miezi 3 Tu

Historia ya Banda na Baroka FC

Abdi Banda mara ya kwanza alijiunga na Baroka FC mnamo Julai 12, 2017, akitokea Simba SC ya Tanzania. Baada ya muda wa mafanikio Afrika Kusini, Banda alirejea Baroka msimu huu wa 2023/2024, akitazamia mchango mkubwa kwa timu hiyo. Hata hivyo, uamuzi wa kuvunja mkataba umekuja baada ya mipango yake ya awali ya kujiunga na Singida Black Stars kugonga mwamba.

Sababu za Kuvunja Mkataba

Kwa mujibu wa wakala wake, Fadhili Omary Sizya, hatua ya kuvunja mkataba ilikuwa ya makubaliano na uongozi wa Baroka FC. Banda alilipa klabu hiyo ili kuhakikisha anaondoka kama mchezaji huru na kuwa na uhuru wa kujiunga na timu nyingine.

“Amevunja mkataba na Baroka na sasa ni mchezaji huru. Ni makubaliano ya pande zote mbili. Kiufupi, aliufuata uongozi akailipa timu na hadi Desemba yuko huru. Sababu ya kufanya hivyo ni kutafuta changamoto sehemu nyingine,” alisema Sizya.

Banda sasa anavutia ofa kutoka klabu kadhaa za Tanzania, ambapo kuna uwezekano mkubwa wa kusaini na moja kati ya timu hizo. Uwezo wake wa kucheza nafasi mbalimbali kama beki wa kati, kushoto, na kiungo mkabaji unamfanya kuwa rasilimali muhimu kwa timu yoyote atakayojiunga nayo.

Kabla ya kurudi Baroka, Banda alihudumu kwa mafanikio katika klabu mbalimbali za Afrika Kusini, ikiwa ni pamoja na Richards Bay, Chippa United, Highlands Park, na TS Galaxy. Katika soka la Tanzania, Banda amewahi kuichezea Coastal Union na Simba SC, ambapo alijizolea umaarufu mkubwa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Winga wa Zamani wa Simba Yusuph Mhilu Atamani Kurejea Ligi Kuu
  2. Dube Afunga Goli 3 na Kuipa Yanga Ushindi Dhidi ya Mashujaa
  3. Washindi wa Tuzo za CAF 2024 (CAF AWARDS 2024)
  4. Msimamo Kundi la Simba Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025
  5. Jackson Shiga Anukia Fountain Gate
  6. Bao la Mwisho la Dube Laipa Yanga Point dhidi ya TP Mazembe
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo