Bado Niponipo Sana tu- Jibu la Tshabalala Kuhusu Kustaafu

Bado Niponipo Sana tu Jibu la Tshabalala Kuhusu Kustaafu

Bado Niponipo Sana tu- Jibu la Tshabalala Kuhusu Kustaafu

Nahodha wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, ameweka wazi msimamo wake kuhusu suala la kustaafu soka, akiendelea kuonyesha kujituma na umakini mkubwa akiwa na kikosi cha Simba kwa zaidi ya misimu 10.

Huku mashabiki wa Simba wakijiuliza iwapo muda wa nahodha huyo kutundika daruga umefika, Tshabalala ametoa kauli yake rasmi, akiwahakikishia kwamba bado yupo imara kuendelea kuchangia mafanikio ya klabu yake.

Bado Niponipo Sana tu- Jibu la Tshabalala Kuhusu Kustaafu

Tshabalala na Mustakabali wa Kustaafu

Tshabalala, ambaye ameweka rekodi ya kucheza katika kiwango cha juu kwa muda mrefu ndani ya kikosi cha Simba, amefafanua kwamba kwa sasa hana mpango wowote wa kustaafu.

Akijibu swali aliloulizwa na Mwanaspoti kuhusu mustakabali wake, nahodha huyo amesema, “Sina wazo kabisa la kustaafu kwa sasa. Kikubwa nina nguvu ya kuisaidia timu, basi ninaweza nikacheza miaka mingi, labda itokee nimepata changamoto ya kuniweka nje.”

Amesisitiza kuwa lengo lake kubwa ni kuendelea kuitumikia timu yake na kujitahidi kadri ya uwezo wake kuhakikisha Simba inazidi kufanya vizuri, huku akionyesha kuwa na uwezo wa kucheza kwa miaka mingi zaidi kama afya na hali yake ya kimwili itaendelea kuwa nzuri.

Siri ya Kuendelea Kuwasha Moto Uwanjani

Tshabalala ametaja nidhamu na bidii katika mazoezi kama nguzo kuu inayomsaidia kudumisha kiwango chake uwanjani. Anasema, “Kinachonifanya nisianguke kiwango ni kuzingatia mazoezi, kujituma, usikivu na kuyafanyia kazi yale ambayo anaelekezwa na makocha. Lakini kubwa zaidi ni kwamba halewi sifa.”

Mbali na mazoezi, Tshabalala amesisitiza umuhimu wa kuzingatia afya na kuepuka tabia zinazoweza kuathiri uwezo wake wa kucheza soka kwa kiwango cha juu. “Siyo kazi rahisi, lakini natambua soka ndio linaloendesha maisha yangu, lazima nijitume na kujitunza. Pia siyo mvivu wa kufanya mazoezi kwa bidii,” aliongeza.

Nje ya Soka: Tshabalala na Kazi ya U-DJ

Kando na soka, Tshabalala amefichua kuwa ana shauku kubwa na kazi ya U-DJ, akibainisha kuwa iwapo asingekuwa mchezaji wa soka, huenda angekuwa DJ maarufu. “Ndio maana nimuumini wa kuwaangalia DJ’s mbalimbali, kwani nisingefanikiwa katika mpira wa miguu, basi ningefanya kazi hiyo,” alisema kwa tabasamu.

Huu ni ushahidi wa jinsi Tshabalala anavyoweza kujiweka imara, siyo tu ndani ya uwanja, bali pia nje ya uwanja, huku akiendelea kuonyesha ufanisi katika mambo mengine anayopenda kufanya.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Fountain Gate FC 2024/2025
  2. Kikosi cha Tanzania Prisons 2024/2025
  3. Wachezaji Wa Yanga Walioitwa Timu ya Taifa October 2024
  4. Wachezaji Wa Simba Walioitwa Timu ya Taifa October 2024
  5. Ratiba ya Mechi za Yanga Ligi Kuu NBC 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo