Baada ya Kibarua Kuota Ndago Yanga, TFF nao Wampiga Pini Gamondi
Baada ya Yanga kutangaza kuachana na aliyekuwa kocha wao mkuu Miguel Gamondi na msaidizi wake Moussa Ndaw leo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limempa adhabu ya kifungo cha mechi tatu na faini ya Sh 2 milioni kutokana na utovu wa nidhamu.
Tangazo hili limekuja katika siku ambayo Gamondi amepata changamoto mbili kubwa, kwanza kuachishwa kazi rasmi na klabu ya Yanga, na pili kufungiwa na TFF kutokana na tukio la utovu wa nidhamu kwenye mechi dhidi ya Singida Black Stars.
Sababu za Kuachana na Gamondi
Taarifa rasmi kutoka Yanga haijataja sababu za moja kwa moja za kuachana na Gamondi, lakini vyanzo vya habari vinaonyesha kuwa hatua hii imechukuliwa kutokana na mwenendo wa timu hiyo msimu huu. Gamondi, ambaye alichukua mikoba ya kuiongoza Yanga, ameshindwa kufikia matarajio ya uongozi na mashabiki wa klabu hiyo.
Adhabu Kutoka TFF
Katika taarifa iliyotolewa na Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi, Gamondi alihusika katika tukio la kumsukuma na kumuangusha kocha wa viungo wa Singida Black Stars, Sliman Marloene, wakati wa mapumziko ya mechi iliyofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
TFF imetumia Kanuni ya 45:2(2.1) ya Udhibiti kwa Makocha wa Ligi Kuu kumchukulia hatua Gamondi kwa:
- Kufungiwa mechi tatu.
- Kulipishwa faini ya Sh 2,000,000.
Tukio hilo limetajwa kama ukiukwaji mkubwa wa maadili ya mchezo wa soka na kutoa mfano wa umuhimu wa nidhamu kwa makocha wa ligi kuu.
Adhabu kwa Singida Black Stars
Pamoja na adhabu dhidi ya Gamondi, klabu ya Singida Black Stars nayo imekumbana na hatua za kinidhamu kwa matukio mawili:
Kuingilia Mazoezi ya Yanga: Singida Black Stars ilivuruga programu ya mazoezi ya Yanga kwa kuingia uwanjani wakati wa muda uliotengwa kwa mazoezi ya Yanga, kinyume na Kanuni ya 17:45 ya Ligi Kuu.
- Adhabu: Faini ya Sh 2,000,000.
Kushindwa Kuheshimu Mahitaji ya Kikao cha Kitaalam cha Maandalizi ya Mchezo (MCM)
Klabu hiyo iliwakilishwa na maafisa wanne pekee badala ya watano kama inavyotakiwa na Kanuni ya 17:2(2.2) ya Ligi Kuu.
- Adhabu: Onyo kali kwa klabu hiyo.
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply