Azam Yatuma Ofa Kwa Simba Kumsajili Kipa Aishi Manula
Klabu ya Azam FC imetuma ofa rasmi kwa Simba SC kwa ajili ya kumsajili kipa wao mahiri, Aishi Manula anaejulikana kwa jina la air Manula kutokana na uhodari wake wa kuchomoa mashuti. Ofa hii inakuja wakati Simba wakiwa na mipango mipya ya kuimarisha safu yao ya ulinzi kwa msimu ujao, huku ikitarajiwa kuwa Ayoub Lakred atakuwa kipa namba moja na Salim ataendelea kuwa kipa namba mbili.
Historia ya Aishi Manula Simba SC
Aishi Manula amecheza kwa mafanikio makubwa akiwa na Simba SC kwa kipindi cha misimu saba, tangu alipojiunga na klabu hiyo mwezi Agosti 2017 akitokea Azam FC. Katika kipindi hicho, Manula amejijengea sifa kama mmoja wa makipa bora zaidi nchini Tanzania, akiweka rekodi za kutosha na kushinda mataji mbalimbali na Simba SC.
Hata hivyo, msimu uliopita haukuwa mzuri kwa Manula kutokana na jeraha la nyonga lililomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu. Hali hii imechangia Azam FC kuona fursa ya kumsajili tena kipa huyo kwa ajili ya kampeni yao ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika.
Mipango ya Azam FC kwa Aishi Manula
Kusajiliwa kwa Aishi Manula na Azam FC ni hatua muhimu kwa wana rambaramba, hasa kwa kuzingatia kuwa wanajiandaa kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika CAF Champions league.
Azam FC imeweka wazi kuwa wana imani kubwa kwa Manula, wakiamini kuwa atatoa ushindani mkubwa kwa kipa wao namba moja, Mohamed Mustafa, ambaye amesaini mkataba mpya baada ya kuonyesha kiwango cha juu msimu uliopita.
Azam FC imeamua kuachana na makipa wao wawili, Abdulai Iddrisu na Ali Ahamada, ambao wamekuwa wakisumbuliwa na majeraha ya muda mrefu. Iddrisu amekuwa akiuguza jeraha la bega, huku Ahamada akisumbuliwa na jeraha la goti. Hali hii imewafanya Azam FC kutafuta mbadala wenye uwezo wa kukabiliana na changamoto za msimu ujao, na Manula ameonekana kuwa chaguo bora.
Kufa kwa Dili la Abuutwalib Mshery
Ujio wa Aishi Manula Azam FC pia umechangia kufa kwa dili la kipa namba mbili wa Yanga, Abuutwalib Mshery, ambaye alikuwa akitajwa kujiunga na Azam FC. Hii ni ishara kuwa Azam FC wameamua kumwekea imani Manula kama kipa wao mpya kwa msimu ujao, wakiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
Mapendekezo Ya Mhariri:
- Tetesi za Usajili simba 2024/2025
- Wachezaji Wapya Yanga | Wachezaji Waliosajiliwa Yanga 2024/2025
- FIFA Yaiondolea Yanga Adhabu ya Kufungiwa Kusajili
- Wachezaji Waliosajiliwa Simba 2024/2025
- Dirisha la Usajili Ligi Kuu Tanzania kufunguliwa Juni 15 hadi Agosti 15, 2024
- Tetesi za Usajili Yanga: Okrah Kwenye Rada za Kuondoka Yanga? Habari Kamili
- Tetesi za Usajili Real Madrid 2024/2025
- Wachezaji Wapya Simba 2024/2025
Leave a Reply