Al Masry Yawasili Dar Kwa Ajili ya Simba – Robo Fainali Kombe la Shirikisho CAF

Al Masry Yawasili Dar Kwa Ajili ya Simba

Al Masry Yawasili Dar Kwa Ajili ya Simba

Kikosi cha Al Masry kutoka nchini Misri tayari kimewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya wenyeji Simba SC. Timu hiyo imefika salama kwa lengo la kutetea ushindi walioupata katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa nchini Misri.

Al Masry Yawasili Dar Kwa Ajili ya Simba – Robo Fainali Kombe la Shirikisho CAF

Katika mchezo huo wa kwanza, Al Masry walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba SC, ushindi ambao umeipa faida timu hiyo inapoelekea kwenye mchezo wa marudiano utakaochezwa Jumatano, Aprili 9, katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Simba SC wanalazimika kushinda kwa tofauti ya mabao zaidi ya mawili bila kuruhusu bao ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa ya ngazi ya klabu Afrika.

Kwa sasa, presha iko kwa kikosi cha Simba SC, ambacho kinatakiwa kuonesha uwezo mkubwa mbele ya mashabiki wao wa nyumbani na kuhakikisha wanaziba pengo la mabao mawili yaliyopatikana katika mchezo wa awali.

Umuhimu wa Mchezo kwa Pande Zote Mbili

Kwa upande wa Al Masry, kuwasili kwao mapema jijini Dar es Salaam kunaonesha dhamira yao ya kupambana na kuhakikisha wanavuka hatua ya robo fainali bila kupoteza mwelekeo. Ushindi wa 2-0 kutoka nyumbani unawapa nafasi nzuri, lakini wanatambua kuwa Simba ni timu ngumu inapocheza nyumbani. Kwa Simba SC, huu ni mchezo wa kufa au kupona. Wanahitaji kushambulia kwa kasi, lakini pia kuwa makini na safu ya ulinzi ili kuepuka kuruhusu bao ambalo linaweza kuwafanya kazi kuwa ngumu zaidi.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Simba Queens Kuachana na Yussif Basigi Mwisho wa Msimu
  2. Rupia Atupia Goli lake la 10 na Kuipa Singida Big Stars Pointi 3 Muhimu Dhidi ya Azam FC
  3. Man United Walazimishwa Sare na Man City Nyumbani Old Trafford
  4. Prince Dube Afukuzia Rekodi Yake Yanga Kimya Kimya
  5. PSG Yatwaa Ubingwa Ligi Kuu Ufaransa 2024/2025 Huku wakiwa Bado na Michezo 6
  6. Mambo Bado Yamoto Ligi Kuu Tanzania
  7. Yanga Yaingia Mawindondi Kuisaka Saini ya Mohamed Omar Ali
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo