Ajira Mpya za Walimu Tanzania 2024: Nafasi 11,015 Zatangazwa, Maombi Hadi Agosti 2

Ajira Mpya za Walimu Tanzania 2024: Nafasi 11,015 Zatangazwa, Maombi Hadi Agosti 2

Serikali ya Tanzania, kupitia Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, imetangaza fursa ya kipekee ya ajira kwa Watanzania wenye sifa. Katika tangazo lake la hivi karibuni, nafasi 11,015 za walimu wapya zimetangazwa wazi, zikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kuimarisha sekta ya elimu nchini. Hii ni fursa ya dhahabu kwa walimu wapya na walimu waliopo ambao wanataka kuboresha nafasi zao za kazi, kuchangia katika ukuaji wa elimu nchini, na kujiimarisha kiuchumi.

Ajira Mpya za Walimu Tanzania 2024: Nafasi 11,015 Zatangazwa, Maombi Hadi Agosti 2

HABARI MPYA: TAARIFA KWA WAOMBAJI NAFASI ZA KAZI KADA ZA UALIMU (14 September 2024)

Ajira Mpya za Walimu Tanzania 2024: Nafasi 11,015 Zatangazwa

Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imeainisha nafasi hizi kama ifuatavyo:

  1. Mwalimu Daraja la IIIA: Nafasi 2,851
  2. Mwalimu Daraja la IIIA – Elimu ya Awali: Nafasi 20
  3. Mwalimu Daraja la IIIA – Elimu Maalum: Nafasi 13
  4. Mwalimu Daraja la IIIB – Shule ya Msingi: Nafasi 464
  5. Mwalimu Daraja la IIIB – Elimu ya Awali: Nafasi 15
  6. Mwalimu Daraja la IIIB – Elimu Maalum: Nafasi 7
  7. Mwalimu Daraja la IIIB – Kemia: Nafasi 488
  8. Mwalimu Daraja la IIIB – Fizikia: Nafasi 740
  9. Mwalimu Daraja la IIIB – Hisabati: Nafasi 663
  10. Mwalimu Daraja la IIIB – Baiolojia: Nafasi 505
  11. Mwalimu Daraja la IIIB – Jiografia: Nafasi 175
  12. Mwalimu Daraja la IIIB – Kiingereza: Nafasi 390
  13. Mwalimu Daraja la IIIB – Fasihi ya Kiingereza: Nafasi 65
  14. Mwalimu Daraja la IIIB – Kiswahili: Nafasi 142
  15. Mwalimu Daraja la IIIB – Historia: Nafasi 152
  16. Mwalimu Daraja la IIIB – Uraia: Nafasi 59
  17. Mwalimu Daraja la IIIB – TEHAMA: Nafasi 59
  18. Mwalimu Daraja la IIIB – Biashara (Bookkeeping): Nafasi 24
  19. Mwalimu Daraja la IIIB – Biashara (Commerce): Nafasi 23
  20. Mwalimu Daraja la IIIB – Kilimo: Nafasi 29
  21. Mwalimu Daraja la IIIB – Kifaransa: Nafasi 2
  22. Mwalimu Daraja la IIIB – Lishe: Nafasi 2
  23. Mwalimu Daraja la IIIB – Ushonaji: Nafasi 2
  24. Mwalimu Daraja la IIIC – Kemia: Nafasi 544
  25. Mwalimu Daraja la IIIC – Fizikia: Nafasi 633
  26. Mwalimu Daraja la IIIC – Hisabati: Nafasi 662
  27. Mwalimu Daraja la IIIC – Baiolojia: Nafasi 515
  28. Mwalimu Daraja la IIIC – Jiografia: Nafasi 310
  29. Mwalimu Daraja la IIIC – Historia: Nafasi 211
  30. Mwalimu Daraja la IIIC – Kiingereza: Nafasi 412
  31. Mwalimu Daraja la IIIC – Kiswahili: Nafasi 184
  32. Mwalimu Daraja la IIIC – Uraia: Nafasi 46
  33. Mwalimu Daraja la IIIC – TEHAMA: Nafasi 33
  34. Mwalimu Daraja la IIIC – Kilimo: Nafasi 31
  35. Mwalimu Daraja la IIIC – Kifaransa: Nafasi 3
  36. Mwalimu Daraja la IIIC – Biashara (Commerce): Nafasi 22
  37. Mwalimu Daraja la IIIC – Biashara (Bookkeeping): Nafasi 19
  38. Mwalimu Daraja la IIIC – Uchumi: Nafasi 16
  39. Mwalimu Daraja la IIIC – Fasihi ya Kiingereza: Nafasi 64
  40. Mwalimu Daraja la IIIC – Shule ya Msingi: Nafasi 37
  41. Mwalimu Daraja la IIIC – Elimu Maalum: Nafasi 3
  42. Fundi Sanifu Maabara ya Shule Daraja la II: Nafasi 380

Masharti na Mwongozo wa Jinsi ya Kutuma Maombi Ajira Mpya za Walimu Tanzania 2024

Watanzania wote wenye sifa zinazohitajika wanahimizwa kuwasilisha maombi yao mapema iwezekanavyo kabla ya tarehe ya mwisho. Maombi yote yanapaswa kuwasilishwa kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’). Waombaji wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanajaza fomu za maombi kwa usahihi na kuambatanisha nyaraka zote muhimu kama ilivyoainishwa katika tangazo la ajira.

Masharti Ya Jumla

  1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
  2. Waombaji wa nafasi za Mwalimu Daraja la III B na Mwalimu Daraja la III C wahakikishe wanambatisha HATI YA MATOKEO (ACADEMIC TRANSCRIPT) katika mfumo wa “Ajira Portal” kwa ajii ya utambuzi wa masomo ya kufundishia.
  3. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  4. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
  5. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  6. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  7. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates. Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI Computer Certificate & Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
  8.  “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  9. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  10. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  11. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  12. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua zakisheria.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamojana vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

  • KATIBU,
  • OFISI YA RAIS,
  • SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
  • L. P. 2320, DODOMA.

Kwa taarifa zaidi kuhusu sifa za kila kada tafadhali pakua tangazo la ajira kupitia tovuti ya TAMISEMI hapa chini.

Bofya Hapa Kupakua

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Nafasi Mpya za Kazi Almashauri ya Wilaya ya Kibiti (Mwisho wa Maombi 28 Julai, 2024)
  2. Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Yatangaza Nafasi za Kazi (Mwisho 25/07/2024)
  3. Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Mbogwe (Mwisho Wa Maombi 26 Julai 2024)
  4. Ajira Mpya Shinyanga: Halmashauri ya Manispaa Yatangaza Nafasi mbalimbali – Mwisho wa Kutuma Maombi ni 25 Julai, 2024
  5. Halmashauri ya Mji Handeni Yatangaza Nafasi Mpya za Kazi (Mwisho Julai 27)
  6. Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi: Mwisho wa Maombi Julai 21, 2024
  7. Mwisho wa Kutuma Maombi Ajira Mpya za Afya Zilizotangazwa July 2024
  8. Nafasi Mpya za Ajira Muuguzi II TAMISEMI 2024: Wauguzi 2282 Wahitaji
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo