Aishi Manula Bado Mambo Magumu Msimbazi
Licha ya kukosekana kwa kipa namba moja wa Simba, Moussa Camara, pamoja na Ally Salim, bado Aishi Manula hakuweza kurejea langoni katika mchezo wa kombe la shirikisho la CRDB dhidi ya Big Man FC uliopigwa jioni ya jana. Hali hii imezua maswali mengi kuhusu nafasi yake ndani ya kikosi cha mabingwa hao wa Tanzania.
Awali, ilitarajiwa kuwa Manula angerudishwa langoni baada ya nyota hao wawili kuachwa nje, lakini badala yake, Hussein Abel aliendelea kupewa nafasi ya kusimama golini. Hili limeongeza utata zaidi kuhusu mustakabali wa mlinda mlango huyo mkongwe ndani ya kikosi cha Msimbazi.
Zaidi ya hilo, jina la Manula halimo katika orodha ya wachezaji waliotangazwa na Simba kusafiri kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry. Huu ni muendelezo wa hali yake ya kutokuonekana kwenye mechi za timu hiyo msimu huu, jambo linaloashiria kuwa nafasi yake kikosini imeendelea kuzidi kuwa finyu.
Manula na Changamoto ya Nafasi Kikosini
Kwa misimu kadhaa, Aishi Manula alikuwa mhimili wa Simba SC na mchango wake ulichangia mafanikio makubwa ya timu hiyo, ikiwemo kutwaa mataji ya Ligi Kuu ya NBC pamoja na kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa. Hata hivyo, mambo yamebadilika haraka, na sasa kipa huyo wa zamani wa Azam FC anaonekana kupoteza nafasi yake ndani ya kikosi cha kwanza cha Simba.
Sababu kuu zinazoelezwa kuathiri nafasi yake ni ujio wa Moussa Camara ambaye ameonyesha kiwango cha juu tangu ajiunge na timu hiyo. Pia, Ally Salim na Hussein Abel wameonekana kuwa chaguo bora kwa benchi la ufundi la Simba, jambo ambalo limezidi kumpunguzia Manula nafasi ya kucheza.
Kwa mujibu wa wachambuzi wa soka, hali hii inaweza kuwa na athari kubwa kwa Manula, hasa ikizingatiwa kuwa ni mmoja wa makipa waliowahi kuwa tegemeo katika kikosi cha Taifa Stars. Kutokupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kunaweza kuathiri kiwango chake na nafasi yake kwenye timu ya taifa, hasa kuelekea michuano mikubwa ya kimataifa inayokuja.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kane Atazamia Kufikia Rekodi ya Shilton na Kuweka Historia Mpya Uingereza
- Yaliyojiri Mkutano wa Waziri Kabudi na TFF, TPLB, Yanga na Simba
- CAF Yaondoa Marufuku Uwanja wa Benjamin Mkapa
- Sowah Aweka Bayana Nia Yake Yakubeba Kiatu Cha Dhahabu
- Majeraha ya Goti Yamkosesha Alphonso Davies Mechi za Mwisho za Msimu
- Yanga Yavamia Dili la Fei Simba
- Silaha 6 Muhimu za Simba SC Zatangulizwa Misri
- Vita ya Top 4 Ligi Kuu Tanzania Bara Yapamba Moto
Leave a Reply