Agosti 8: Haji Manara Awaonya Simba SC Dhidi ya Kuleta Timu Uwanjani

Haji Manara Awaonya Simba SC Dhidi ya Kuleta Timu Uwanjani

Agosti 8: Haji Manara Awaonya Simba SC Dhidi ya Kuleta Timu Uwanjani

Katika maandalizi ya pambano la Ngao ya Jamii linalotarajiwa kufanyika Agosti 8, msemaji wa Yanga SC, Haji Manara, ametoa onyo kali kwa wapinzani wao Simba SC. Manara ameonya kuwa Simba SC wasijaribu kuleta timu yao uwanjani kwani watajikuta wanakutana na maumivu makali kutoka kwa Yanga SC. Kauli hii imekuja baada ya Yanga sc kuonesha kiwango cha hali ya juu katika  michezo yao iliofanyika Afrika kusini katika michuano ya kombe la Toyota na Mpumalanga Premier’s International Cup.

Haji Manara Awaonya Simba SC Dhidi ya Kuleta Timu Uwanjani

Timu Imara ya Yanga SC

Haji Manara amesisitiza kuwa Yanga SC ina timu imara ambayo imeboreshwa zaidi kwa kuongeza wachezaji mahiri. “Tuna Chama, tuna Pacome. Tutawafunga Simba SC si chini ya bao 4,” alisema Manara kwa kujiamini. Yanga SC inaendelea na kocha yule yule ambaye ameiongoza timu kwa mafanikio makubwa, tofauti na Simba SC ambao wamesajili timu mpya.

Onyo kwa Mashabiki na Wachezaji wa Simba SC

Manara amewataka mashabiki wa Simba SC kuwa waangalifu na kuacha ukaidi wa kwenda uwanjani siku hiyo. Aliwaonya kuwa watakutana na maumivu ikiwa watashikilia kwenda kushuhudia pambano hilo. “Wachezaji kila ukiwauliza wanasema wao wanawaza Agosti 8 tu. Baleke ana hasira yani waambieni Agosti 08 wasilete timu uwanjani,” aliongeza Manara.

Historia ya Mtanange wa Ngao ya Jamii

Simba SC na Yanga SC zinatarajiwa kukutana katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Ngao ya Jamii, pambano linaloashiria kufunguliwa kwa msimu mpya. Katika mechi ya mwisho baina ya timu hizi mbili, Simba SC ilipoteza kwa mabao 2-1. Pia, katika mzunguko wa kwanza wa msimu wa 2023/24, Simba SC ilichapwa na Yanga SC kwa mabao 5-1, jambo ambalo linaongeza mzuka wa pambano hili la Agosti 8.

Angalia Hapa Maojiano yote Ya Haji Manara na Waandishi wa Habari

Hitimisho

Kwa kauli yake, Haji Manara ameweka wazi kuwa Yanga SC imejipanga kikamilifu kwa ajili ya pambano la Ngao ya Jamii na wamejidhatiti kuhakikisha kuwa wanawapa mashabiki wao furaha ya ushindi.

Simba SC wanapaswa kuchukua onyo hili kwa uzito na kufanya maandalizi ya ziada ikiwa wanataka kuepuka aibu mbele ya Yanga SC. Agosti 8 itakuwa siku ya kihistoria kwa mashabiki wa soka nchini Tanzania.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Yusuph Kagoma kuikosa Kariakoo Dabi
  2. Simba SC Yafunga Pre-season kwa Ushindi
  3. Matokeo Simba Vs Al Adalah FC Leo (29/07/2024)- Mechi ya Kirafiki
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo