Timu Zinazoshiriki Kombe la Muungano 2025
AZIA la michuano ya Kombe la Muungano linafunguliwa rasmi Alhamisi hii, tarehe 24 Aprili 2025, kwa mchezo wa robo fainali kati ya JKU SC dhidi ya Singida Black Stars. Mchezo huo utachezwa saa 11:00 jioni katika Uwanja wa Gombani, kisiwani Pemba.
Singida Black Stars ni miongoni mwa timu nane zilizofanikiwa kufuzu kushiriki michuano hiyo msimu huu, nafasi waliyopata baada ya Simba kujitoa kutokana na ratiba ngumu ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Michuano hii ya Kombe la Muungano, inayorejea kwa mwaka wa pili mfululizo tangu kurejeshwa kwake mwaka 2024 baada ya kupotea kwa takribani miaka 22, inawakutanisha wakali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar katika ushindani mkali wa soka unaolenga kudumisha mshikamano wa kitaifa na kukuza vipaji.
Timu Washiriki
Kwa msimu wa 2025, jumla ya timu nane zinashiriki michuano hii, zikigawanyika kutoka pande mbili za Muungano:
Timu Zinazoshiriki Kombe la Muungano 2025 Kutoka Tanzania Bara:
- Azam FC
- Coastal Union SC
- Singida Black Stars SC
- Young Africans SC (Yanga)
Timu Zinazoshiriki Kombe la Muungano 2025 Kutoka Zanzibar:
- JKU SC
- KMKM SC
- KVZ FC
- Zimamoto SC
Kila timu inaingia kwenye mashindano haya ikiwa na azma ya kutwaa taji la Kombe la Muungano kwa mara ya kwanza, kwani hakuna hata moja iliyowahi kushinda taji hili tangu michuano hii ianze mwaka 1982.
Historia Fupi na Hadhi ya Michuano
Kombe la Muungano limekuwa sehemu muhimu ya historia ya soka la Tanzania, likilenga kuunganisha wanamichezo kutoka pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano. Katika historia ya taji hili, Yanga SC na Simba SC ndizo zenye mafanikio makubwa zaidi, kila moja ikiwa imetwaa taji hilo mara sita. Hata hivyo, msimu huu Simba haipo katika mashindano hayo baada ya kujitoa kutokana na majukumu ya kimataifa.
Mabingwa watetezi ni Simba SC, waliotwaa taji hilo mwaka 2024. Michuano ya mwaka huu inatoa fursa kwa timu nyingine kuandika historia mpya kwa kulitwaa taji hili kwa mara ya kwanza.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya Kombe la Muungano 2025
- Yanga Yaishushia Fountain Gate Kichapo Cha 4-0 na Kuweka Rekodi
- Kikosi cha Yanga VS Fountain Gate Leo 21/04/2025
- Matokeo ya Fountain Gate vs Yanga Leo 21/04/2025
- Fountain Gate FC vs Yanga Leo 21/04/2025 Saa Ngapi?
- Ifahamu Jayrutty Investment Company Limited, Mdhamini Mpya wa Simba
- Dickson Ambundo Ajiondoa Fountain Gate Akidai Kutolipwa Zaidi ya Shilingi Milioni 50
- Viingilio Mechi ya Simba VS Stellenbosch 20/04/2025
- Vituo Vya Kununua Tiketi Mechi ya Simba VS Stellenbosch 20/04/2025
Leave a Reply