Simba VS Stellenbosch Leo 20/04/2025 Saa Ngapi?

Simba VS Stellenbosch Leo 20 04 2025 Saa Ngapi

Simba VS Stellenbosch Leo 20/04/2025 Saa Ngapi?

Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, kinatarajiwa kushuka dimbani leo Jumapili, Aprili 20, 2025, kwa ajili ya kuumana na Stellenbosch FC ya Afrika Kusini katika mechi ya kwanza ya hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mchezo huo wa kihistoria utapigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar kuanzia saa 10:00 jioni, baada ya Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kufungiwa kwa ajili ya ukarabati unaoendelea.

Kwa mara ya kwanza, mchezo wa hatua kubwa ya mashindano ya CAF unachezwa visiwani Zanzibar, jambo linaloongeza uzito wa tukio hili. Aidha, hii ni mara ya kwanza kwa timu zote mbili—Simba na Stellenbosch—kufuzu hatua ya nusu fainali ya Kombe hili, na kila moja ikiwa tayari imewahi kuwavua ubingwa mabingwa watetezi.

Simba VS Stellenbosch Leo 20/04/2025 Saa Ngapi?

Tiketi na Bei za Viingilio

Kwa mashabiki wanaotaka kushuhudia mchezo huu muhimu, tiketi zimeanza kuuzwa rasmi katika vituo mbalimbali. Bei za viingilio ni kama ifuatavyo:

  • VIP A: Shilingi 40,000
  • VIP B: Shilingi 20,000
  • Mzunguko: Shilingi 10,000

Ahmed Ally ametoa wito kwa mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi na kuisapoti timu yao kwa maombi na uwepo wa kimwili, huku akisisitiza umuhimu wa kutunza amani na nidhamu ili kuendelea kutoa taswira chanya kwa Tanzania kwenye michuano ya CAF.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Dickson Ambundo Ajiondoa Fountain Gate Akidai Kutolipwa Zaidi ya Shilingi Milioni 50
  2. Viingilio Mechi ya Simba VS Stellenbosch 20/04/2025
  3. Vituo Vya Kununua Tiketi Mechi ya Simba VS Stellenbosch 20/04/2025
  4. Kikosi cha Stellenbosch Chawasili Zanzibar kwa Ajili ya Simba
  5. Ratiba ya Mechi za Leo 19/04/2025 Ligi Kuu NBC
  6. Msigwa Afunguka Kuhusu Ukarabati wa Uwanja wa Mkapa
  7. Polisi Tanzania Yajipanga Kulpa Kisasi Dhidi ya Mbeya City Babati
  8. Ifahamu Jayrutty Investment Company Limited, Mdhamini Mpya wa Simba
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo