Dickson Ambundo Ajiondoa Fountain Gate Akidai Kutolipwa Zaidi ya Shilingi Milioni 50

Dickson Ambundo Ajiondoa Fountain Gate Akidai Kutolipwa Zaidi ya Shilingi Milioni 50

Dickson Ambundo Ajiondoa Fountain Gate Akidai Kutolipwa Zaidi ya Shilingi Milioni 50

KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Fountain Gate, Dickson Ambundo, ameondoka rasmi katika kikosi cha timu hiyo akidai kutolipwa malimbikizo ya fedha, ikiwemo zaidi ya Shilingi milioni 50 zinazodaiwa kuwa ni sehemu ya fedha za usajili.

Ambundo, ambaye alijiunga na Fountain Gate mwanzoni mwa msimu huu akitokea Singida Black Stars, amehusika katika kuifungia timu hiyo mabao mawili kabla ya kujiondoa kambini huku ligi ikielekea ukingoni kwa raundi nne tu zilizobakia.

Katika mazungumzo yake na Mwanaspoti, Ambundo alithibitisha kutokuwapo kwenye kikosi cha timu hiyo, akibainisha kuwa sababu kuu ni malimbikizo ya mishahara pamoja na stahiki nyingine ambazo hajalipwa na waajiri wake.

“Ni kweli sipo pamoja na timu kwa sababu nina madai na timu hiyo na tayari nimepeleka malalamiko yangu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kupambania haki yangu,” alisema Ambundo, ambaye amewahi pia kuzichezea klabu za Alliance, Yanga na Dodoma Jiji.

Dickson Ambundo Ajiondoa Fountain Gate Akidai Kutolipwa Zaidi ya Shilingi Milioni 50

Kwa mujibu wa mchezaji huyo, hatua ya kuwasilisha malalamiko yake TFF inalenga kutafuta haki kwa njia ya kisheria, kwa kuwa juhudi za ndani ya klabu hazikuzaa matunda. Ambundo ameweka wazi kuwa hatua yake haikulenga kuvuruga hali ya kikosi, bali ni matokeo ya kutolipwa haki zake za msingi kwa muda mrefu.

Hata hivyo, uongozi wa klabu ya Fountain Gate kupitia kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wake, Kidawawa Tabitha, umekanusha vikali tuhuma hizo za kutodaiwa na Ambundo. Akizungumza na Mwanaspoti, Tabitha alisisitiza kuwa Ambundo bado ni mchezaji halali wa Fountain Gate, na kwamba sababu pekee ya kutokuwapo kwake kambini ni matatizo ya kiafya.

“Taarifa hizo hazina ukweli wowote. Ambundo bado ni mchezaji wetu halali, yupo nje ya timu kwa sababu anaugua, na hiyo ndiyo taarifa tuliyonayo. Kuhusu kuidai klabu, hiyo taarifa ndiyo kwanza nakusikia wewe,” alieleza Tabitha.

Kauli hizi mbili zinazotofautiana zimeibua sintofahamu kuhusu hatma ya kiungo huyo ndani ya kikosi cha Fountain Gate. Wakati Ambundo akisisitiza kuwa ameondoka rasmi kwa sababu ya kutolipwa zaidi ya Shilingi milioni 50, uongozi wa klabu unasisitiza kuwa bado ana mkataba halali na anasubiri kurejea baada ya kupona.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Viingilio Mechi ya Simba VS Stellenbosch 20/04/2025
  2. Vituo Vya Kununua Tiketi Mechi ya Simba VS Stellenbosch 20/04/2025
  3. Kikosi cha Stellenbosch Chawasili Zanzibar kwa Ajili ya Simba
  4. Ratiba ya Mechi za Leo 19/04/2025 Ligi Kuu NBC
  5. Msigwa Afunguka Kuhusu Ukarabati wa Uwanja wa Mkapa
  6. Polisi Tanzania Yajipanga Kulpa Kisasi Dhidi ya Mbeya City Babati
  7. Ifahamu Jayrutty Investment Company Limited, Mdhamini Mpya wa Simba
  8. Wafungaji Bora CRDB Bank Federation Cup 2024/2025
  9. Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Klabu bingwa UEFA Champions 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo