Viingilio Mechi ya Simba VS Stellenbosch 20/04/2025
Wachezaji wa Stellenbosch Football Club wamewasili visiwani Zanzibar kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali ya mashindano ya CAF Confederation Cup dhidi ya wenyeji wao, Simba SC ya Tanzania. Mchezo huo wa kusisimua unatarajiwa kupigwa siku ya Jumapili, tarehe 20 Aprili 2025, katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar, kufuatia kufungwa kwa Uwanja wa Benjamin Mkapa kupisha ukarabati.
Kwa upande wa Simba SC, kikosi chao kilitua visiwani hapo mapema zaidi, mnamo Aprili 16, 2025, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo wa kwanza wa nusu fainali. Mchezo huu ni muhimu kwa klabu hiyo ambayo inalenga kuandika historia kwa kufuzu fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.
Viingilio Rasmi kwa Mchezo
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, tiketi za mchezo huo zimeanza kuuzwa rasmi. Bei za viingilio vimepangiliwa kama ifuatavyo:
- VIP A: TSh 40,000
- VIP B: TSh 20,000
- Mzunguko: TSh 10,000
Ahmed amebainisha kuwa tiketi zinapatikana katika vituo vyote rasmi vya uuzaji na amewahimiza mashabiki kujitokeza kwa wingi kununua tiketi mapema ili kuepuka usumbufu siku ya mchezo.
Malengo ya Simba SC: Fainali na Zaidi
Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Aprili 15, 2025, Ahmed Ally alieleza kuwa Simba SC haijiandai kwa mechi hii kama hatua ya mwisho, bali kama daraja la kuelekea fainali ya CAF Confederation Cup. Ameeleza kuwa timu hiyo imejipanga kuhakikisha inatumia vyema faida ya kucheza nyumbani ili kupata matokeo mazuri kabla ya mchezo wa marudiano.
Ahmed alisisitiza kuwa Stellenbosch si timu ya kubezwa, kwani kufika kwao nusu fainali si kwa bahati bali ni kwa uwezo wao mkubwa wa kiuchezaji. Aliwataka wachezaji wa Simba kuwa makini na kujituma katika dakika zote tisini za mchezo huo ili kuibuka na ushindi wa maana.
“Tuna kazi ya kumdhibiti na kumfunga mpinzani wetu katika uwanja wa nyumbani kwa lengo la kuimaliza kazi yetu mapema tukiwa kwetu,” alisema Ahmed.
Wito kwa Mashabiki: Maombi, Amani na Nidhamu
Mbali na kueleza mikakati ya Simba kuelekea fainali, Ahmed aliwahimiza mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuiombea timu yao kwa njia wanayoamini, huku wakidumisha nidhamu na amani ndani na nje ya uwanja. Aliongeza kuwa mwenendo mzuri wa mashabiki ni sehemu muhimu ya mafanikio ya timu katika mashindano ya kimataifa kama haya.
“Inawezekana Simba kucheza fainali kwani timu tunayo na tumejipanga vizuri kuandika historia hiyo mwaka huu ikiwa mikononi mwetu,” alisema kwa msisitizo.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Vituo Vya Kununua Tiketi Mechi ya Simba VS Stellenbosch 20/04/2025
- Kikosi cha Stellenbosch Chawasili Zanzibar kwa Ajili ya Simba
- Ratiba ya Mechi za Leo 19/04/2025 Ligi Kuu NBC
- Msigwa Afunguka Kuhusu Ukarabati wa Uwanja wa Mkapa
- Polisi Tanzania Yajipanga Kulpa Kisasi Dhidi ya Mbeya City Babati
- Ifahamu Jayrutty Investment Company Limited, Mdhamini Mpya wa Simba
Leave a Reply