Polisi Tanzania Yajipanga Kulpa Kisasi Dhidi ya Mbeya City Babati

Polisi Tanzania Yajipanga Kulpa Kisasi Dhidi ya Mbeya City Babati

Polisi Tanzania Yajipanga Kulpa Kisasi Dhidi ya Mbeya City Babati

Timu ya Polisi Tanzania inatarajiwa kushuka dimbani siku ya Ijumaa, Aprili 18, 2025, kuikabili Mbeya City katika mchezo wa kusisimua wa Ligi ya Championship utakaopigwa katika Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa, mjini Babati.

Huu ni mchezo unaobeba uzito wa kipekee kwa kikosi cha Polisi Tanzania, si tu kwa sababu ya pointi muhimu tatu, bali pia kwa dhamira ya kulipiza kisasi dhidi ya wapinzani wao waliowashinda katika duru la kwanza.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Polisi Tanzania, Inspekta Frank Lukwaro, kikosi hicho kimejiandaa vyema kwa mtanange huo muhimu, kikiwa na malengo ya kuhakikisha ushindi unapatikana na kuendeleza matumaini ya kupanda daraja au kubaki kileleni mwa msimamo. Lukwaro amesema kuwa kikosi kipo imara bila majeruhi, hali inayowapa nguvu zaidi kuelekea pambano hilo.

Polisi Tanzania Yajipanga Kulpa Kisasi Dhidi ya Mbeya City Babati

“Tunatambua kuwa tulifungwa katika mzunguko wa kwanza kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, lakini mchezo huu ni nafasi ya kurekebisha makosa na kulipa kisasi. Kila mchezaji amedhamiria kupambana kwa nguvu kuhakikisha tunapata alama tatu muhimu,” alisema Lukwaro kwa msisitizo.

Katika kutambua umuhimu wa sapoti ya mashabiki, Inspekta Lukwaro ametoa wito kwa wakazi wa Babati na mashabiki wa Polisi Tanzania kufika kwa wingi uwanjani siku ya Ijumaa ili kuiunga mkono timu yao. Amesisitiza kuwa mchezo huo unachezwa siku ya mapumziko, hivyo ni fursa nzuri kwa mashabiki kuonyesha mshikamano wao na kutoa hamasa kwa wachezaji.

Kwa upande wa mashabiki na wadau wa soka nchini, hii ni nafasi ya kushuhudia moja ya michezo ya ushindani mkubwa katika Ligi ya Championship msimu huu, ambapo Polisi Tanzania wanaingia na ari mpya, dhamira ya ushindi, na kiu ya kulipa kisasi dhidi ya Mbeya City.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ifahamu Jayrutty Investment Company Limited, Mdhamini Mpya wa Simba
  2. Wafungaji Bora CRDB Bank Federation Cup 2024/2025
  3. Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Klabu bingwa UEFA Champions 2024/2025
  4. Simba SC Yasaini Mkataba Mnono wa Vifaa vya Michezo
  5. Ratiba ya CRDB Federation Cup Fixtures 2024/2025
  6. Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking)
  7. Matokeo ya Yanga vs Stand United Leo 15/04/2025
  8. Kikosi cha Yanga vs Stand United Leo 15/04/2025
  9. Viingilio Mechi ya Yanga SC VS Stand United Leo 15/04/2025
  10. Yanga VS Stand United Leo 15/04/2025 Saa Ngapi?
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo