Ifahamu Jayrutty Investment Company Limited, Mdhamini Mpya wa Simba

Ifahamu Jayrutty Investment Company Limited Mdhamini Mpya wa Simba

Ifahamu Jayrutty Investment Company Limited, Mdhamini Mpya wa Simba

Klabu ya Simba SC imeingia rasmi kwenye ushirikiano wa kihistoria kwa kusaini mkataba wa miaka mitano na Kampuni ya Jayrutty Investment Company East African Limited, wenye thamani ya Shilingi bilioni 38.

Mkataba huo unalenga utengenezaji, ubunifu na usambazaji wa vifaa vya michezo vya klabu hiyo, ikiwa ni hatua ya kimkakati katika kuinua ubora wa miundombinu na maendeleo ya soka ndani ya timu hiyo maarufu barani Afrika.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Tenda ya Simba SC, Dkt. Seif Muba, mchakato wa kumpata mzabuni ulifanyika kwa uwazi, ukihusisha makampuni mbalimbali yaliyowasilisha maombi. Jayrutty Investment Company Limited ilichaguliwa baada ya kutimiza vigezo vyote vilivyowekwa, na kutoa ahadi ya faida kubwa kwa klabu katika kipindi chote cha mkataba.

Ifahamu Jayrutty Investment Company Limited, Mdhamini Mpya wa Simba

Thamani ya Mkataba na Mafao kwa Simba SC

Dkt. Muba alifafanua kuwa Kampuni ya Jayrutty Investment itakuwa inatoa Shilingi bilioni 5.6 kwa mwaka, kiasi ambacho kitaongezeka kwa asilimia 10 kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano ya mkataba. Hili linaifanya Simba SC kuwa miongoni mwa klabu chache za Afrika zilizoingia mikataba yenye manufaa ya muda mrefu kifedha.

Aidha, CPA Joseph Rwegasira, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Jayrutty Investment, alieleza kuwa mbali na thamani ya kifedha ya mkataba huo, Simba itanufaika kwa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na:

  • Ujenzi wa uwanja wa kisasa utakaoingiza mashabiki 10,000 hadi 12,000
  • Ununuzi wa basi la kisasa la Irizar kwa matumizi ya timu
  • Ujenzi wa ofisi za kudumu za klabu
  • Uanzishaji wa studio ya kisasa kwa ajili ya kurusha maudhui ya habari za Simba SC

Zaidi ya hapo, kampuni hiyo itatoa Shilingi milioni 100 kila mwaka kwa ajili ya kukuza soka la vijana, pamoja na kiasi kingine cha milioni 100 kwa maandalizi ya msimu mpya (Pre-Season). Motisha kwa wachezaji pia imezingatiwa kwa kutengwa Shilingi milioni 470 kila mwaka kwa kipindi chote cha miaka mitano ya mkataba.

Kuhusu Jayrutty Investment Company Limited

Jayrutty Investment Company East African Limited ni kampuni inayojivunia ubunifu, ubora na uimara wa vifaa vya michezo kwa ajili ya wachezaji wa ngazi zote. Lengo lake kuu ni kuwawezesha wanamichezo kwa kutumia vifaa vya kisasa vinavyoinua viwango vyao vya ushindani.

Kwa mujibu wa taarifa za kampuni hiyo, jayrutty investment company limited inajihusisha na utoaji wa huduma mbalimbali kama zifuatazo:

  1. Vifaa vya Timu za Michezo: mipira ya miguu, mpira wa kikapu, wavu, milingoti ya magoli, nyavu, na koni za mazoezi.
  2. Vifaa vya Riadha: vifaa vya mbio, vizuizi vya mazoezi, na vifaa vya kuanzia mbio.
  3. Vifaa vya Fitness na Mazoezi: mikanda ya resistance, dumbbells, vifaa vya mazoezi ya gym, ngazi za agility, na vifaa vya kuongeza kasi.
  4. Michezo ya Shule na Burudani: vifaa vya uwanja kwa matumizi ya wanafunzi na taasisi za elimu.

Kwa kuzingatia ubora, teknolojia ya kisasa, na dhamira ya kuhakikisha kila bidhaa inapita kwenye vipimo vya hali ya juu, Jayrutty imejiweka katika nafasi bora ya kuwa mdau mkuu wa maendeleo ya michezo katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Makao Makuu

Jayrutty Investment Company Limited inapatikana katika ghorofa ya saba ya jengo la Morocco Square Office Tower, barabara ya Mwai Kibaki, Regent Estate, Kinondoni – Dar es Salaam. Eneo hili ni la kimkakati, likiwa karibu na taasisi mbalimbali za michezo na biashara, na linalowezesha kampuni hiyo kufikia wadau wake kwa ufanisi mkubwa.

Kwa Taarifa Zaidi Kuhusu Jayrutty Investment Company Limited tembelea tovuti yao rasmi kupitia kiungo ww.jayruttyinvestment.com

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Wafungaji Bora CRDB Bank Federation Cup 2024/2025
  2. Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Klabu bingwa UEFA Champions 2024/2025
  3. Simba SC Yasaini Mkataba Mnono wa Vifaa vya Michezo
  4. Ratiba ya CRDB Federation Cup Fixtures 2024/2025
  5. Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking)
  6. Matokeo ya Yanga vs Stand United Leo 15/04/2025
  7. Kikosi cha Yanga vs Stand United Leo 15/04/2025
  8. Viingilio Mechi ya Yanga SC VS Stand United Leo 15/04/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo