Clement Mzize: Mfungaji Bora Kombe la Shirikisho la CRDB Bank 2024
Baada ya michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania ambalo hujulikana kama CRDB baank federation Cup kumalizika jun 3 2024 kwa fainali iliyohusisha mabingwa wa ligi kuu ya NBC Tanzania Yanga Sc Dhidi ya Azam Fc ambapo Yanga ilishinda kwa mikwaju ya penati kwa goli 6-5. Baada ya kumalizika kwa michuano hii sasa na pazia la dirisha la ufungaji bora nalo limefungwa rasmi. Kama wewe ni shabiki wa soka Tanzania na ungependa kujua wafungaji bora wa CRDB Bank federation Cup basi umekuja mahali sahihi.
Mfungaji Bora Kombe la Shirikisho la CRDB Bank 2024
Mfungaji bora wa michuano ya Kombe la shirikisho la CRDB kwa mwaka 2024 ni mshambuliaji kinda kutoka Yanga Sc Clement Mzize. Mzize bila shaka amekua na msimu mzuri uku akiwa na jumla ya magoli 5 katika michezo 6 ya kombe la shirikisho.
Ingawa Mzize ametajwa kuwa ndio mfungaji bora katika michuano ya CRDB bank federation cup 2024, ushindani haukuwa mdogo. Edward Songo wa JKT Tanzania alikuwa mpinzani wake mkubwa, akiwa amefunga mabao 5 sawa na alofunga Mzize. Hata hivyo, kanuni za michuano zinasema kuwa endapo wachezaji wawili watakuwa na idadi sawa ya mabao, mchezaji ambaye timu yake imefika mbali zaidi ndiye atakayetangazwa mshindi. Kwa bahati mbaya, JKT Tanzania iliondolewa mapema kwenye michuano, na hivyo kumpa Mzize ushindi.
Wachezaji Wengine Waliofanya Vizuri Katika Mbio za Ufungaji Bora CRDB Bank federation Cup
Ingawa Clement Mzize ndio mfungaji bora wa michuano ya Kombe la shirikisho kwa mwaka 2024, wachezaji wengine kadhaa walionyesha umahiri wao katika kupachika magoli. Abdul Suleiman ‘Sopu’ wa Azam FC na Yohana Mkomola wa Tabora United walifunga mabao 4 kila mmoja, wakishika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji bora wa Kombe la shirikisho CRDB Bank 2024.
Kundi la wachezaji waliofunga mabao 3 kila mmoja lilikuwa na ushindani mkali, likijumuisha Joseph Guede wa Young Africans, Sadio Kanoute wa Simba SC, Kelvin Sabato wa Namungo FC, George Chande wa TMA Stars, Francis Joseph wa Mkwajuni FC, George Komba wa Rhino Rangers, Shaban Seif wa Mbuni FC, na Wagana Paskas wa Biashara United.
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply