Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Kombe la FA Uingereza 2024/2025
Hatimaye miamba manne itakayoshiriki hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA Uingereza imejulikana baada ya mechi kali za robo fainali kumalizika. Mashindano haya ya kihistoria yameendelea kuwa yenye ushindani mkali, huku timu zikipambana vikali kutafuta nafasi ya kutwaa taji hilo lenye historia kubwa katika ulimwengu wa soka Uingereza.
Manchester City, ambao walitwaa ubingwa wa FA mwaka 2023, walifuzu kwa hatua hii baada ya ushindi wa kusisimua dhidi ya Bournemouth. Nottingham Forest, kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1991, walipenya hadi nusu fainali baada ya ushindi wa mikwaju ya penalti dhidi ya Brighton. Aston Villa waliendeleza ubabe wao kwa kuichabanga Preston kwa mabao 3-0, huku Crystal Palace wakifanikisha safari yao kwa ushindi mnono wa 3-0 dhidi ya Fulham.
Hizi ndizo Timu zilizofuzu hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la FA Uingereza 2024/2025
- Manchester City
- Nottingham Forest
- Aston Villa
- Crystal Palace
Hatua ya nusu fainali inatarajiwa kuwa ya kusisimua, huku kila timu ikipania kufika fainali. Mechi hizi zitachezwa mwishoni mwa wiki ya tarehe 26 Aprili kwenye Uwanja wa Wembley, ambapo mashabiki wanatarajia burudani ya kiwango cha juu.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Haaland na Marmoush Waipeleka Man City Nusu Fainali FA Cup
- Nyota Wa Real madrid Hatiani Kuikosa Robo fainali UEFA Dhidi ya Arsenal
- Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2024/2025
- Kikosi Cha Simba kilichosafiri kwenda misri kucheza dhidi ya Al Masry
- Yanga SC Yatinga Robo Fainali Kombe la FA Baada ya Kuichapa Songea United
- Kikosi cha Yanga vs Songea United Leo 29/03/2025
- Yanga vs Songea United Leo 29/03/2025 Saa Ngapi?
Leave a Reply