Tabora United Kuwakabili JKT Tanzania CCM Kirumba Machi 7, 2025

Tabora United Kuwakabili JKT Tanzania CCM Kirumba

Tabora United Kuwakabili JKT Tanzania CCM Kirumba Machi 7, 2025

Siku tano baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutangaza kufungiwa kwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, uongozi wa Tabora United umechagua Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kuwa mwenyeji wa mchezo wake wa nyumbani dhidi ya JKT Tanzania utakaochezwa Machi 7, 2025.

Katika taarifa rasmi iliyotolewa na klabu hiyo, Tabora United imethibitisha kuwa mechi hiyo ya Ligi Kuu ya NBC itaanza saa 16:00 jioni, huku mashabiki wakihimizwa kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao.

Hatua ya kuhamishia mchezo huo CCM Kirumba inafuatia uamuzi wa TFF kuufungia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kwa kutokidhi viwango vya kikanuni vinavyohitajika kwa michezo ya Ligi Kuu. Uwanja huo umegundulika kuwa na miundombinu mibovu, ikiwemo nyasi zilizokauka, hali iliyotajwa kuathiri ubora wa mchezo.

Uongozi wa Tabora United umewahakikishia mashabiki wake kuwa juhudi zinaendelea kufanywa kwa kushirikiana na serikali ya mkoa na wadau mbalimbali ili kuhakikisha Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi unaboreshwa na kufunguliwa kwa matumizi ya mechi zilizobaki za Ligi Kuu.

Tabora United Kuwakabili JKT Tanzania CCM Kirumba

Matokeo ya Tabora United Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi

Kwa misimu iliyopita, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi umekuwa ngome muhimu kwa Tabora United, ambapo msimu huu pekee wamecheza michezo 11, wakishinda mara tano, kutoka sare mara nne, na kupoteza michezo miwili. Ushindi wao wa mwisho katika uwanja huo ulikuwa dhidi ya Dodoma Jiji FC, ambapo walishinda bao 1-0 kabla ya kutangazwa kwa adhabu ya kufungiwa kwa uwanja huo.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Bodi ya Ligi TPLB Yatangaza Tarehe Mpya ya Mechi ya Simba na Dodoma
  2. Timu Zilizofuzu 16 Bora Kombe la Shirikisho la CRDB Federation Cup 2024/2025
  3. Mechi za Yanga Zilizobaki Ligi Kuu NBC 2024/2025
  4. Ratiba ya Kombe la Shirikisho la CRDB Federation Cup Leo 03/03/2025
  5. Ratiba ya Mechi za Simba Machi 2025
  6. Mbeya City Yaing’oa Azam CRDB Bank Federation Cup kwa Mikwaju ya Penati
  7. Simba Yaivuruga Rekodi ya Mwambusi Arusha
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo