Kikosi cha Simba vs Coastal Union Leo 01/03/2025 | Kikosi cha Simba leo Dhidi ya Coastal Union
Kikosi cha Simba leo kitashuka dimbani kuwakabili Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Huu ni mchezo muhimu kwa pande zote mbili, huku Simba SC ikihitaji ushindi ili kuendelea kuwania ubingwa, wakati Coastal Union wakisaka alama tatu zitakazowaweka katika nafasi salama kwenye msimamo wa ligi.
Simba inakabiliwa na presha kubwa ya kuhakikisha haipotezi alama ili kufukuzia Yanga SC, ambayo inaongoza ligi. Katika msimamo wa ligi, Yanga SC ilikuwa na alama 58 kabla ya mechi yao dhidi ya Pamba Jiji, huku Simba ikiwa na alama 51 na michezo miwili mkononi. Ushindi leo utawapa nafasi ya kupunguza tofauti ya pointi na kuweka matumaini ya kurudisha ubingwa walioukosa kwa misimu mitatu mfululizo.
Kwa upande wa Coastal Union, wanahitaji ushindi ili kujiweka salama katikati ya msimamo wa ligi. Kwa sasa wana alama 24 baada ya michezo 21, na matokeo mabaya leo yanaweza kuwaweka katika hatari ya kushuka daraja. Mechi ya kwanza ya msimu huu kati ya timu hizi ilimalizika kwa sare ya 2-2, jambo linaloashiria kuwa pambano la leo litakuwa na ushindani mkubwa.
Kikosi cha Simba vs Coastal Union Leo 01/03/2025
Kikosi rasmi cha Simba kitakachoshuka dimbani leo kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 9:00 alasiri. Tutakuletea orodha kamili ya wachezaji mara tu kocha Faldu Davis atakapokitangaza. Tegemea mchezo wenye ushindani na muto wa kipee, ambapo Yanga itaendelea kuimarisha nafasi yake kileleni, huku Mashujaa Fc ikipambana kuendelea kujihimarisha katika nafasi za juu za msimamo wa ligi.
Rekodi ya Mechi za Hivi Karibuni
Katika michezo yao 10 ya mwisho, Simba imeshinda mara 7 dhidi ya Coastal Union, huku Coastal wakifanikiwa kupata sare 3. Simba ina rekodi nzuri ya kufunga mabao dhidi ya Coastal, ikiwa imefunga jumla ya mabao 24 katika mechi hizo 10, wakati Coastal wakifunga mabao 5 pekee.
Katika mchezo wa msimu wa 2021/2022, Simba iliiadhibu Coastal Union kwa mabao 7-0 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, matokeo ambayo bado yapo kwenye kumbukumbu za mashabiki wa timu zote mbili. Hata hivyo, Coastal imeimarika na leo wanatarajia kufanya vizuri zaidi.
Wachezaji wa Kutazamwa
Kwa upande wa Simba, washambuliaji Jean Charles Ahoua mwenye mabao 10 na Lionel Ateba mwenye mabao 8 wanatarajiwa kuwa panga kali katika safu ya ushambuliaji. Kwa upande wa Coastal, mshambuliaji Maabad Maabad ndiye kinara wa mabao wa timu hiyo akiwa na mabao 5, akifuatiwa na Abdallah Hassan mwenye mabao 2, ambaye pia alifunga dhidi ya Simba kwenye sare ya 2-2.
Simba italazimika kucheza bila kipa wao namba moja Moussa Camara na beki Che Malone Fondoh walioumia katika mechi yao dhidi ya Azam. Hili linaweza kuwa pigo kwa Wekundu wa Msimbazi, lakini watalazimika kutumia kikosi chao cha nyota wengine kama Aishi Manula au Ally Salim golini ili kuhakikisha wanadhibiti mashambulizi ya Coastal.
Mikakati ya Timu Kwa Mchezo wa Leo
Kocha wa Simba, Fadlu Davids, amesisitiza kuwa wanahitaji ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa. Ameeleza kuwa Coastal Union ni timu yenye nidhamu na wachezaji mahiri, hivyo wataingia kwa tahadhari kubwa kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
Kwa upande wa Coastal, kocha Juma Mwambusi amesisitiza kuwa wanajua ubora wa Simba lakini pia wanajua udhaifu wao, hivyo wamejiandaa kupambana ili kupata ushindi muhimu. Coastal ina rekodi nzuri ya safu ya ulinzi, ikiwa imefungwa mabao matatu tu katika michezo mitano ya mwisho huku wakicheza mechi tatu bila kuruhusu bao.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Coastal Union Vs Simba Leo 01/03/2025 Saa Ngapi?
- Mashujaa FC Yathibitisha Kumfuta Kazi Kocha Mohamed Abdallah ‘Baress’
- Arajiga Kuchezesha Mechi ya Kufuzu Kombe La Dunia 2026
- Twiga Stars Yavuka Raundi ya Pili WAFCON Baada ya Sare Dhidi ya Guinea
- Antony Afutiwa Kadi Nyekundu, Sasa Ruksa Kuivaa Madrid
- Matokeo ya Equatorial Guinea vs Twiga Star Leo 26/02/2024
- Man United Wamnyemelea Xavi Kuchukua Mikoba ya Amorim
Leave a Reply