Kikosi cha Yanga vs Mashujaa Leo 23/02/2025 | Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya Mashujaa Fc
Timu ya Wananchi, Yanga SC, leo itakuwa ugenini kuwakabili Mashujaa FC katika Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma. Mechi hii itaanza kutimua vumbi majira ya saa 10:15 jioni na inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na nafasi ya timu hizo kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Ushindi kwa timu yoyote utakuwa na athari kubwa kwenye kampeni zao za msimu huu
Mechi hii ni ya muhimu kwa Yanga SC na Mashujaa FC kwa sababu tofauti. Kwa Yanga, ushindi utawafanya waendelee kuongoza ligi kwa kufikisha pointi 55. Pia, utawapa utulivu kuelekea mchezo wao mkubwa wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba SC Machi 8, baada ya kucheza mechi moja dhidi ya Pamba FC. Kushinda pia kutawaongezea shinikizo Simba SC ambao wapo nyuma kwa tofauti ya pointi mbili na wanakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Azam FC Jumatatu.
Kwa upande wa Mashujaa FC, ushindi utawapandisha kutoka nafasi yao ya sasa hadi nafasi ya sita kwa kufikisha pointi 26. Hata hivyo, iwapo watapoteza au kutoka sare, wataendelea kuwa katika mazingira hatarishi ya kushuka daraja kwani wana tofauti ya pointi tano pekee dhidi ya timu zilizo mstari wa kushuka daraja. Kwa hiyo, mechi hii ni muhimu kwa Mashujaa ili kujihakikishia nafasi salama kwenye msimamo wa ligi.
Kikosi cha Yanga vs Mashujaa Leo 23/02/2025
Kikosi rasmi cha Yanga kitakachoshuka dimbani leo kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 9:15 alasiri. Tutakuletea orodha kamili ya wachezaji mara tu kocha Miloud Hamdi atakapokitangaza. Tegemea mchezo wenye ushindani na muto wa kipee, ambapo Yanga itaendelea kuimarisha nafasi yake kileleni, huku Mashujaa Fc ikipambana kuendelea kujihimarisha katika nafasi za juu za msimamo wa ligi.
Wachezaji wa Kuzingatia Katika Mechi Hii
Mashujaa FC wanamtegemea mshambuliaji wao hatari, David Ulomi, ambaye mpaka sasa amefunga mabao manne katika msimu huu wa Ligi Kuu. Ulomi amejijengea jina kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kupiga mashuti ya mbali, hivyo Yanga italazimika kuwa makini kumzuia.
Kwa upande wa Yanga SC, safu yao ya ushambuliaji imekuwa kali msimu huu. Wachezaji wanaoongoza kwa kufumania nyavu ni Clement Mzize, ambaye anaongoza katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu akiwa na mabao 10, na Prince Dube, ambaye amefunga mabao tisa. Hawa ni wachezaji wa kutazamwa kwa karibu na safu ya ulinzi ya Mashujaa FC.
Takwimu za Msimu Huu
Yanga SC imeonyesha kiwango bora wanapocheza ugenini msimu huu. Katika mechi tisa walizocheza ugenini, wamekusanya pointi 25 kwa kushinda mechi nane na kutoka sare moja. Kwa upande wa Mashujaa FC, wamekuwa na matokeo mseto katika uwanja wao wa nyumbani. Katika mechi 10 walizocheza Lake Tanganyika msimu huu, wameshinda mechi nne, wametoka sare nne na wamepoteza mbili.
Kauli za Makocha Kabla ya Mchezo
Kocha wa Yanga SC, Hamdi Miloud, ameweka wazi kuwa wamekuja Kigoma kwa lengo moja tu – ushindi. Alisema, “Tunajua mechi hii itakuwa ngumu, tunawajua wapinzani wetu na tunawaheshimu. Hatupo hapa kupumzika, lengo letu ni kushinda na kuchukua pointi tatu dhidi ya Mashujaa.”
Kwa upande wake, kocha wa Mashujaa FC, Mohamed Abdallah ‘Baresi’, alisema kuwa wanajua wanacheza dhidi ya timu kubwa yenye wachezaji wenye uwezo wa kuamua matokeo. Alisema, “Tumejipanga vizuri kuhakikisha tunawapa upinzani mkubwa Yanga SC. Tunafahamu hatupo salama kwenye msimamo wa ligi, kwa hiyo tunahitaji pointi ili kujiepusha na hatari ya kushuka daraja.”
Ratiba Nyingine ya Ligi Kuu Leo
Kabla ya mchezo kati ya Mashujaa FC na Yanga SC, kutakuwa na mechi nyingine mbili za Ligi Kuu. Mechi ya kwanza itaanza saa 8:00 mchana kati ya Singida Black Stars na Pamba Jiji FC kwenye Uwanja wa CCM Liti, Singida. Mchezo wa mwisho kwa siku ya leo utapigwa saa 1:00 usiku baina ya Namungo FC na Coastal Union kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, Lindi.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Washindi wa Tuzo za Wachekeshaji Tanzania 2025
- Droo Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika CAF 2025
- Droo Robo Fainali Kombe la Shirikisho 2025
- Droo ya Robo Fainali CAF Kombe la Shirikisho & Klabu Bingwa (Februari 20 2025)
- Wapinzani wa Simba Robo Fainali Kombe la Shirikisho CAF
- Matokeo ya Namungo Vs Simba Leo 19/02/2025
- Kikosi cha Simba Vs Namungo Leo 19/02/2025
Leave a Reply