Droo Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika CAF 2025

Droo Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika CAF 2025

Droo Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika CAF 2025

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limeendesha droo rasmi ya hatua ya robo fainali kwa michuano ya Klabu Bingwa Afrika msimu wa 2024/25. Droo hiyo, iliyofanyika tarehe 20 Februari, imefanyika moja kwa moja kutoka katika studio za kisasa za beIN SPORTS, washirika wa haki za matangazo ya CAF, jijini Doha, Qatar. Droo hiyo imekuja na mechi nne za kukatana shoka zitakazoshuhudia timu nane bora barani Afrika zikichuana katika mechi za mikondo miwili ili kupata nafasi ya kufuzu kwa hatua ya nusu fainali.

Michezo ya Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika CAF 2025

Katika droo hii, mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly SC kutoka Misri, watakabiliana na Al Hilal SC ya Sudan katika mechi inayotarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa. Al Ahly, ambao wameshinda taji hili mara 12, wanapambana kuweka historia kwa kushinda taji hili kwa mara ya tatu mfululizo.

Al Hilal, inayonolewa na Florent Ibengé kutoka DR Congo, iliongoza kundi lake licha ya changamoto ya kucheza mechi zake za nyumbani nchini Mauritania kutokana na mgogoro unaoendelea Sudan. Timu hiyo inajivunia safu ya ulinzi imara itakayojaribu kuzuia mashambulizi ya mabingwa hao watetezi.

Katika mchezo mwingine wa kusisimua, klabu ya Pyramids FC ya Misri itakutana na mabingwa wa Morocco, AS FAR. Pyramids, inayoongozwa na Kocha Krunoslav Jurčić wa Croatia, iliibuka na safu ya ushambuliaji yenye makali makubwa baada ya kufunga mabao 14 katika hatua ya makundi, kiwango sawa na klabu nyingine iliyofunga mabao mengi zaidi. AS FAR, chini ya kocha wao wa Kireno, Alexandre Santos, waliweza kuvuka hatua ya makundi bila kupoteza mchezo wowote, wakionyesha uimara wao.

Katika pambano jingine kali, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini watavaana na Esperance Sportive de Tunis ya Tunisia. Mamelodi Sundowns, mabingwa wa mwaka 2016, wanajaribu kuvunja mwiko wa kutolewa katika nusu fainali, hatua ambayo wamekwama mara nyingi tangu walipotwaa ubingwa. Kwa upande wao, Esperance, mabingwa mara nne wa Ligi ya Mabingwa Afrika, waliibuka kinara wa kundi lao na wanatoka kutwaa taji la Super Cup ya Tunisia chini ya Kocha Laurențiu Reghecampf kutoka Romania.

Nayo MC Alger ya Algeria, ambayo ilikuwa na rekodi bora ya ulinzi kwa kuruhusu mabao mawili pekee katika hatua ya makundi, itapambana na Orlando Pirates ya Afrika Kusini. Orlando Pirates, mabingwa wa mwaka 1995, waliongoza kundi lao kwa alama 14 na wanatafuta nafasi ya kufika nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu walipomaliza kama washindi wa pili mwaka 2013. Kwa upande wao, MC Alger, inayoongozwa na kocha Khaled Ben Yahia kutoka Tunisia, inajivunia safu imara zaidi ya ulinzi kwenye michuano hiyo.

Ratiba ya Mechi za Robo Fainali

  • QF 1: Al Ahly SC (Misri) vs Al Hilal SC (Sudan)
  • QF 2: Pyramids FC (Misri) vs AS FAR (Morocco)
  • QF 3: Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) vs Esperance Sportive de Tunis (Tunisia)
  • QF 4: MC Alger (Algeria) vs Orlando Pirates (Afrika Kusini)

Droo Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika CAF 2025

Droo ya Hatua ya Nusu Fainali

Baada ya droo ya robo fainali, upangaji wa mechi za nusu fainali pia ulifanyika.

  • SF 1: Mshindi wa Mamelodi Sundowns vs Esperance atakutana na mshindi wa Al Ahly SC vs Al Hilal SC.
  • SF 2: Mshindi wa MC Alger vs Orlando Pirates atakutana na mshindi wa Pyramids FC vs AS FAR.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Droo Robo Fainali Kombe la Shirikisho 2025
  2. Droo ya Robo Fainali CAF Kombe la Shirikisho & Klabu Bingwa (Februari 20 2025)
  3. Wapinzani wa Simba Robo Fainali Kombe la Shirikisho CAF
  4. Matokeo ya Namungo Vs Simba Leo 19/02/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo