Mwisho wa Kutuma Maombi Nafasi za Kazi TRA Februari 2025
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitangaza nafasi 1,596 za ajira kwa wahitimu wa elimu na fani mbalimbali, ikiwakaribisha Watanzania wenye sifa na uwezo kutuma maombi yao kwa nafasi mbalimbali zilizotangazwa. Nafasi hizi zinajumuisha sekta tofauti ndani ya TRA, zikiwemo Idara ya Mapato ya Ndani, Forodha na Ushuru, Usimamizi na Utawala wa Rasilimali Watu, Huduma za Sheria, Menejimenti ya Manunuzi, Utafiti na Mipango, Fedha, Ukaguzi wa Ndani, Mambo ya Ndani pamoja na Idara ya Vihatarishi na Uzingatiaji.
Nafasi za Kazi Zilizotangazwa
TRA imetangaza nafasi katika kada mbalimbali ikiwa ni pamoja na:
- Ofisa Msimamizi Ushuru daraja la II – Nafasi 573
- Ofisa Forodha daraja la II – Nafasi 232
- Msaidizi wa Usimamizi wa Ushuru daraja la II – Nafasi 253
- Msaidizi wa Forodha daraja la II – Nafasi 154
- Mhadhiri Msaidizi – Nafasi 15
- Ofisa Usimamizi Data daraja la II – Nafasi 20
- Ofisa Rasilimali Watu daraja la II – Nafasi 11
- Ofisa Utawala daraja la II – Nafasi 3
- Ofisa Usafirishaji daraja la II – Nafasi 5
- Ofisa Milki daraja la II – Nafasi 15
- Wahandisi daraja la II – Nafasi 12
- Wajiolojia daraja la II – Nafasi 2
- Ofisa Hesabu daraja la II – Nafasi 12
- Mhasibu daraja la II – Nafasi 2
- Ofisa Mambo ya Ndani daraja la II – Nafasi 10
- Ofisa Vihatarishi daraja la II – Nafasi 8
- Wachumi daraja la II – Nafasi 6
- Watakwimu daraja la II – Nafasi 4
- Mwanasheria daraja la II – Nafasi 6
- Ofisa Manunuzi na Usambazaji daraja la II – Nafasi 5
- Ofisa Maabara – Nafasi 3
- Mkutubi daraja la II – Nafasi 4
- Ofisa Taaluma daraja la II – Nafasi 2
- Mkaguzi wa Ndani daraja la II – Nafasi 2
- Mlinzi daraja la II – Nafasi 2
- Ofisa Uhusiano daraja la II – Nafasi 5
- Msaidizi wa Mafunzo – Nafasi 2
- Katibu Muhtasi daraja la II – Nafasi 12
- Mtaalamu wa Maabara daraja la II – Nafasi 4
- Ofisa Hesabu Msaidizi – Nafasi 10
- Msaidizi wa Usimamizi wa Rekodi daraja la II – Nafasi 10
- Mafundi Uashi na Umeme daraja la II – Nafasi 10
- Mwendesha Mfumo wa Ulinzi daraja la II – Nafasi 9
- Nahodha daraja la II – Nafasi 8
- Fundi Boti – Nafasi 8
- Mkutubi Msaidizi daraja la II – Nafasi 2
- Nahodha Msaidizi daraja la II – Nafasi 2
- Mtu wa Mapokezi daraja la II – Nafasi 20
- Dereva daraja la II – Nafasi 105
- Msaidizi wa Ofisi daraja la II – Nafasi 27
Mwisho wa Kutuma Maombi
TRA imeweka wazi kuwa mwisho wa kutuma maombi kwa nafasi zote za ajira zilizotangazwa ni leo, tarehe 19 Februari 2025 saa tana na dakika 59 usiku. Waombaji wanaohitaji nafasi hizi na bado hawajawasilisha maombi yao wanashauriwa kuhakikisha kuwa wamekamilisha mchakato wa maombi kwa muda uliopangwa ili kuepuka changamoto zozote za muda wa mwisho.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Nafasi za Kazi Jeshi la Zimamoto 2025
- Mfano wa Barua Ya Maombi ya Kazi Jeshi la Zimamoto 2025
- Mfumo wa Maombi ya Ajira Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (Zimamoto Ajira Portal)
- Nafasi za Kazi Ualimu MDAs NA LGAs February 2025
- Mfumo wa Kutuma Maombi ya Ajira TRA (TRA recruitment Portal Login)
- Nafasi za Kazi TRA Februari 2025: Ajira Zaidi ya 1000 kwa Fani Mbalimbali
- Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Kada ya Ualimu 2025 Mikoa Mbalimbali
- Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi TRA (Tanzania Revenue Authority)
- Majina waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo Jeshi la Uhamiaji 2025
Leave a Reply