Matokeo ya JKT Tanzania Vs Yanga Leo 10/02/2025 | Matokeo ya Yanga leo Dhidi ya JKT Tanzania
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania, Yanga SC, leo wanakutana na wenyeji JKT Tanzania katika dimba la Meja Jenerali Isamuhyo liliopo Mbweni jijini Dar Es Salaam kwenye mchezo wa raundi ya pili wa ligi kuu. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, kwa kuwa timu zote zinahitaji pointi tatu muhimu.
Kwa Yanga SC, ushindi ni muhimu ili kuendelea kuongoza msimamo wa ligi na kuongeza nafasi ya kutwaa ubingwa kwa mara ya nne mfululizo. Kwa sasa, Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 45 baada ya kushinda mechi 15 na kupoteza mbili kati ya michezo 17. Wanafuatiwa kwa karibu na Simba SC wenye pointi 44. Kwa upande wa JKT Tanzania, timu hiyo imekusanya jumla ya pointi 19 katika michezo 17, na wanahitaji ushindi ili kujinasua kutoka katika eneo la hatari la kushuka daraja.
Katika mchezo wa raundi ya kwanza kati ya timu hizi uliofanyika katika Uwanja wa Azam Complex, Yanga ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania. Matokeo hayo yanawapa Yanga ari ya kutaka kurudia mafanikio hayo leo, huku JKT Tanzania wakipania kulipiza kisasi na kulinda heshima yao mbele ya mashabiki wao.
Matokeo ya JKT Tanzania Vs Yanga Leo 10/02/2025
JKT Tanzania | 0-0 | Yanga Sc |
- JKT TANZANIA vs YANGA SC
- Tarehe: 10/02/2025
- Uwanja: MEJA GENERAL ISAMUYO
- Muda: saa 10:00 jioni
Kauli za Makocha
Kocha wa Yanga SC, Miloud Hamdi, alisisitiza kuwa wanatarajia mchezo mgumu lakini wanafanya maandalizi kuhakikisha wanapata alama tatu. “Tunatambua kuwa tutakuwa na mchezo mgumu, lakini tutafanya juhudi kubwa kuhakikisha tunapata alama tatu. JKT Tanzania ni timu nzuri, tunajua wanapenda kucheza soka safi, hivyo tutajiandaa kupambana,” alisema Miloud Hamdi.
Kwa upande mwingine, benchi la ufundi la JKT Tanzania limeweka mkazo kwenye nidhamu ya uchezaji na utulivu ndani ya uwanja.
“Tunahitaji kuwa bora zaidi uwanjani kwa sababu tunacheza na timu yenye ubora mkubwa. Tutahakikisha tunakuwa watulivu na tunatumia nafasi tunazopata kwa ufanisi,” ilielezwa kutoka kwa benchi la ufundi la JKT Tanzania.
Rekodi ya Timu Hadi Sasa
JKT Tanzania ina rekodi isiyoridhisha katika mechi tano za mwisho, wakipata sare mbili na kupoteza mechi tatu mfululizo. Timu hiyo ilifungwa 2-1 na Coastal Union na 3-1 na Azam FC katika mechi zao za hivi karibuni. Kwa upande wa msimu mzima, JKT Tanzania imefanikiwa kushinda mechi nne pekee, wakifunga mabao 11 na kufungwa 14.
Hata hivyo, JKT Tanzania imeonyesha uimara katika mechi za nyumbani, ambapo wameshinda michezo mitatu na kutoka sare nne. Wanatumaini kutumia faida ya uwanja wa nyumbani ili kuwashangaza wageni wao, Young Africans.
Kwa upande wa Yanga SC, mabingwa hao wamekuwa na msimu bora zaidi, wakiwa wameshinda michezo saba mfululizo ya ligi. Wamekuwa na rekodi ya kufunga mabao mengi huku wakiruhusu magoli machache. Katika michezo yao miwili iliyopita, Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Kengold na 4-0 dhidi ya Kagera Sugar.
Pia, Yanga imekuwa na rekodi bora ya michezo ya ugenini, wakishinda mechi saba mfululizo msimu huu.
Kikosi Rasmi cha Yanga Vs JKT Tanzania Leo
Kikosi cha Yanga kitakachoshuka dimbani leo kinatarajiwa kutangazwa rasmi majira ya saa 9:00 alasiri. Mara baada ya kutangazwa, tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wa pande zote mbili. Fuatilia Taarifa kuhusu ikosi hapa Kikosi cha Yanga vs JKT Tanzania Leo 10/02/2025
Mapendekezo ya Mhariri:
- Bao la Kaseke Laipa Pamba Ushindi Dhidi ya Azam FC
- Ushindi Dhidi ya Dodoma Jiji Wampa Jeuri Minziro
- Ngassa: Mechi dhidi ya Simba itakuwa ngumu, lakini tunajua pakupenya
- KenGold Yaahidi Kujifuta Machozi ya 6-1 Mbele ya Fountain Gate
- Ratiba ya Mechi za Tanzania (Taifa Stars) Afcon 2025
- CAF Yatangaza Ratiba Ya Fainali za Afcon 2025
- Droo ya Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2024/2025 Hatua ya 32 & 16 Bora
- Matokeo ya Simba vs Fountain Gate Leo 06 Februari 2025
Leave a Reply