Matokeo ya Yanga vs Kengold Leo 05/02/2025 | Matokeo ya Yanga leo dhidi ya Kengold Ligi Kuu ya NBC
NBC Premier League leo inashuhudia pambano la kukata na shoka kati ya Yanga SC na KenGold FC katika dimba la KMC Complex, Mwenge. Mchezo huu unaotarajiwa kuanza saa 10:15 jioni, unawakutanisha mabingwa watetezi wa ligi kuu na timu inayoshika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi. Je, Yanga itaendelea na mwenendo wake wa ushindi, au KenGold itapata alama muhimu katika harakati zake za kusalia ligi kuu?
Kikosi cha Yanga SC kinaingia katika mchezo huu kikiwa na morali ya juu baada ya ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja huu huu wa KMC Complex. Ushindi huo uliwafanya Yanga kupanda hadi kileleni mwa msimamo wa ligi kwa muda, wakifikisha rekodi ya ushindi wa mechi sita mfululizo chini ya kocha wao, Sead Ramovic.
Katika ushindi wao wa mwisho, nyota wao waliotikisa nyavu ni Clement Mzize, Pacome Zouzoua, Mudathir Yahya, na Kennedy Musonda Romelu. Lengo lao kuu leo ni kuendeleza rekodi nzuri kwa kupata ushindi wa saba mfululizo.
Akizungumzia mchezo huu, kocha Ramovic alisema wanajipanga kutumia ipasavyo nafasi wanazozipata, huku akisisitiza kuwa hawatawabeba wapinzani wao licha ya kuwa nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi.
“Tunaendelea na harakati za kulinda ubingwa wetu. Ushindi dhidi ya KenGold ni muhimu, na tunapaswa kuwa makini kwenye ulinzi na umakini kwenye mashambulizi,” alisema Ramovic.
Kwa upande wa KenGold, hali yao si shwari kwani bado wanashikilia mkia kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama sita pekee baada ya michezo 16. Wanakutana na Yanga wakiwa na rekodi mbaya ya kufungwa mechi nne mfululizo, jambo linalowafanya kuwa katika hatari kubwa ya kushuka daraja.
KenGold walijaribu kuimarisha kikosi chao katika dirisha dogo la usajili kwa kufanya mabadiliko makubwa, wakisajili wachezaji wazoefu kama Bernard Morrison (aliyewahi kuchezea Yanga na Simba), Obrey Chirwa, Zawadi Mauya, na Kelvin Yondani. Hata hivyo, Morrison hataweza kushiriki mchezo wa leo kutokana na majeraha.
Mbali na mabadiliko ya wachezaji, KenGold pia walifanya mabadiliko ya benchi la ufundi kwa kumleta kocha mpya, Vladislav Heric, ambaye ni kocha wao wa nne msimu huu. Heric ana jukumu zito la kuiokoa timu hiyo na kuhakikisha inapata matokeo chanya dhidi ya Yanga.
Matokeo ya Yanga vs Kengold Leo 05/02/2025
Yanga Sc | VS | Kengold Fc |
🔰TAARIFA ZA MECHI🔰
- 🏆 #NBCPremierLeague
- ⚽️ Young Africans SC🆚Kengold SC
- 📆 05.02.2025
- 🏟 KMC Complex
- 🕖 10:15 Jioni
Historia ya Mechi Zao
Mchezo wa leo ni wa mzunguko wa 17 wa ligi, huku timu hizi zikiwa tayari zilikutana kwenye raundi ya kwanza Septemba 25, 2024, katika uwanja wa Sokoine, Mbeya. Katika mchezo huo, Yanga ilishinda kwa bao 1-0, na leo wanapewa nafasi kubwa ya kushinda tena kutokana na ubora wa kikosi chao na hali mbaya ya KenGold.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi cha Yanga vs Kengold Leo 05/02/2025
- Yanga vs Kengold Leo 05/02/2025 Saa Ngapi?
- CV ya Miloud Hamdi, Kocha Mpya wa Yanga 2025
- Timu zilizofuzu 32 bora CRDB Bank Federation Cup 2024/2025
- Vinara wa Assist NBC Premier League 2024/2025
- Matokeo ya Yanga Vs Kagera Sugar Leo 01/02/2025
- Ratiba ya Mechi za Yanga February 2025
- Kikosi cha Yanga Vs Kagera Sugar Leo 01/02/2025
- Aliekua Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi Atua Al Nasr ya Libya
- Kagera Sugar Yatamba Kuondoa Unyonge KMC Complex Dhidi ya Yanga
- Morocco Aweka Mikakati ya Ushindi dhidi ya Vigogo Ndani ya Kundi C AFCON 2025
Leave a Reply