Kikosi cha Yanga vs Kengold Leo 05/02/2025 | Kikosi cha Yanga leo dhidi ya Kengold Ligi Kuu
Katika dimba la KMC Complex leo jioni, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Young Africans SC (Yanga), watashuka dimbani kuvaana na Kengold SC katika mchezo wa raundi ya 17 ya NBC Premier League. Mchezo huu unatajwa kuwa na mvuto wa kipekee, ukizikutanisha timu mbili zilizo kwenye hali tofauti – Yanga ikiwa kinara wa ligi huku Kengold ikiburuza mkia.
Baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Kagera Sugar wiki iliyopita, Yanga imeendelea kuonesha ubabe wake chini ya kocha Sead Ramovic. Ushindi huo uliifanya timu hiyo kufikisha ushindi wa sita mfululizo, ikiwa na malengo ya kuendeleza rekodi hiyo kwa mchezo wa leo. Wachezaji kama Clement Mzize, Pacome Zouzoua, Mudathir Yahya, na Kennedy Musonda Romelu wameonesha uwezo mkubwa na wanatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya kikosi kitakachopambana dhidi ya Kengold.
Kwa upande mwingine, Kengold SC ipo katika hali mbaya baada ya kupoteza michezo minne mfululizo kwenye ligi. Ikiwa na pointi sita pekee baada ya mechi 16, timu hiyo inakabiliwa na hatari ya kushuka daraja ikiwa haitabadilisha mwenendo wake. Ili kuimarisha kikosi chao, Kengold ilifanya mabadiliko makubwa katika dirisha dogo la usajili, ikiwajumuisha wachezaji wenye uzoefu kama Bernard Morrison, Obrey Chirwa, na Kelvin Yondani. Pia, wameajiri kocha mpya, Vladislav Heric, katika jitihada za kubadili matokeo yao mabaya.
Kikosi cha Yanga vs Kengold Leo 05/02/2025
Kikosi rasmi cha Yanga kitakachoshuka dimbani leo kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 9:00 alasiri. Tutakuletea orodha kamili ya wachezaji mara tu kocha Miloud Hamdi atakapokitangaza. Tegemea mchezo wenye ushindani na muto wa kipee, ambapo Yanga itaendelea kuimarisha nafasi yake kileleni, huku Kengold ikipambana kujinasua kutoka kwenye janga la kushuka daraja.
Je, Kengold Wanaweza Kushangaza?
Kwa kuzingatia ubora wa kikosi cha Yanga na mwenendo wa Kengold katika michezo kadhaa iliopita, mabingwa watetezi wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huu tena kwa zaidi ya mmagoli matatu. Hata hivyo, Kengold, ikiwa na wachezaji wapya na kocha mpya, inaweza kupambana vikali ili kuzuia kuendelea kuporomoka zaidi katika msimamo wa ligi.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Yanga vs Kengold Leo 05/02/2025 Saa Ngapi?
- CV ya Miloud Hamdi, Kocha Mpya wa Yanga 2025
- Vinara wa Assist NBC Premier League 2024/2025
- Aliekua Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi Atua Al Nasr ya Libya
- Makundi ya Fainali za Mataifa ya Afrika AFCON 2025
- Kundi la Taifa Stars AFCON 2025
- Msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) 2024/2025
- Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier League
Leave a Reply