Matokeo ya Yanga Vs Kagera Sugar Leo 01/02/2025 | Matokeo ya Yanga Dhidi ya Kagera Sugar Leo
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya NBC, Yanga SC, leo wanakipiga na Kagera Sugar katika uwanja wa KMC Complex, Mwenge jijini Dar es Salaam. Mechi hii ni ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania bara na imepangwa kuanza kutimua vumbi majira ya saa 10 jioni.
Yanga, wenye hasira baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League), wanahitaji ushindi ili kuendelea kuifukuzia Simba kwenye msimamo wa ligi. Je, wataweza kuendleza ubabe wao dhidi ya Kagera Sugar?
Yanga Yahitaji Pointi Tatu Muhimu
Kama Yanga itashinda mchezo wa leo itafikisha pointi 42 na kuipiku Simba, ambao wana pointi 40. Hata hivyo, Simba wanaweza kuipoka Yanga nafasi hiyo ikiwa watafanikiwa kushinda mechi yao inayofuata, kwani watafikisha pointi 43. Yanga, ambao wanatafuta taji la nne mfululizo, wanahitaji kushinda ili kuendelea kuwa na matumaini ya kutwaa ubingwa.
Chini ya kocha Sead Ramovic, Yanga imekuwa na rekodi bora kwenye mechi zake tano zilizopita za ligi, ikishinda zote na kufunga mabao 18 huku ikiruhusu mawili pekee. Timu hiyo inaonekana kuwa na safu kali ya ushambuliaji, inayoongozwa na Clement Mzize mwenye mabao sita, Pacome Zouzoua aliye na mabao sita pia, na Prince Dube mwenye mabao matano.
Kwa upande mwingine, Kagera Sugar ina hali ngumu kwenye msimamo wa ligi, ikiwa nafasi ya 15 kwa pointi 11 pekee. Katika mechi tano zilizopita, Kagera Sugar imeambulia sare tatu na kupoteza mechi mbili, hali inayowafanya kupambana ili kujinasua kutoka mkiani.
Ikiwa Kagera itaweza kushinda mechi hii, itapanda hadi nafasi ya 13 huku ikisubiri matokeo ya timu nyingine. Hata hivyo, rekodi dhidi ya Yanga haiko upande wao, kwani katika mechi 10 zilizopita baina ya timu hizi, Kagera Sugar haijawahi kupata ushindi wowote dhidi ya Yanga, isipokuwa sare mbili tu.
Matokeo ya Yanga Vs Kagera Sugar Leo 01/02/2025
Yanga Sc | VS | Kagera Sugar |
- 🏆 #NBCPremierLeague
- ⚽️ Young Africans SC🆚Kagera Sugar
- 📆 01.02.2025
- 🏟 KMC Complex
- 🕖 10:00 Jioni
Maandalizi ya Timu zote Mbili
Kocha wa Yanga, Sead Ramovic, ameeleza kuwa kikosi chake kimejiandaa kikamilifu kwa mchezo huu na lengo ni kuhakikisha wanapata ushindi ili kufanikisha malengo yao ya kutetea ubingwa. “Hatufanyi makosa, tunahitaji ushindi katika kila mechi ya mzunguko wa pili,” alisema Ramovic.
Kwa upande wa Kagera Sugar, kocha Mellis Medo amesisitiza kuwa wachezaji wake wako tayari kwa changamoto na watahakikisha hawaruhusu bao la mapema. “Tunajua Yanga ni timu yenye uzoefu mkubwa, lakini tutajitahidi kuwadhibiti na kutafuta nafasi ya kushinda,” alisema Medo. Katika mechi hii, Kagera Sugar haitamtumia mshambuliaji wao mpya George Mpole, kwani bado hajaungana na timu kikamilifu. Hata hivyo, wamepata nguvu mpya kwa kusajili kipa Ahmed Feruzi na kiungo Mkenya, Shaphan Siwa.
Rekodi za Yanga Vs Kagera Sugar za Hivi Karibuni
Katika mechi 10 za mwisho kati ya Yanga na Kagera Sugar, Yanga imeshinda mechi 8 na mbili zikiisha kwa sare. Katika michezo hiyo, Yanga imefunga jumla ya mabao 18 huku Kagera ikifunga mabao matatu pekee. Mara ya mwisho timu hizi zilipokutana msimu huu, Yanga ilishinda kwa mabao 2-0 katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi cha Yanga Vs Kagera Sugar Leo 01/02/2025
- Aliekua Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi Atua Al Nasr ya Libya
- Kagera Sugar Yatamba Kuondoa Unyonge KMC Complex Dhidi ya Yanga
- Morocco Aweka Mikakati ya Ushindi dhidi ya Vigogo Ndani ya Kundi C AFCON 2025
- Simba SC Yajiandaa Vikali Kuisambaratisha Tabora United
- Makundi ya Fainali za Mataifa ya Afrika AFCON 2025
- Tanzania Yapangwa Kundi C AFCON 2025
- Timu zilizofuzu 32 bora CRDB Bank Federation Cup 2024/2025
- Ramovic Aelezea Sababu za Ikanga Kukosa Mchezo wa Kombe la Shirikisho
- Lyanga Apania Kufanya Makubwa Mashujaa FC
- Kagera Sugar Yatangaza Kumsajili Feruzi Kutoka Simba
Leave a Reply