Kikosi cha Yanga Vs Kagera Sugar Leo 01/02/2025 | Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya Kagera Sugar 01 februari 2025
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, leo wanashuka dimbani kuvaana na Kagera Sugar katika Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam. Mchezo huu wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara unatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni, huku Yanga ikisaka ushindi muhimu ili kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi.
Iwapo Yanga itashinda leo, itafikisha pointi 42 na kuipiku Simba SC yenye pointi 40, lakini kama Simba itashinda mechi yake kesho, itaipita Yanga kwa pointi moja na kurejea kileleni. Hili linafanya ushindi kwa Yanga kuwa wa lazima ili kuweka hai matumaini ya kutetea ubingwa wake kwa mara ya nne mfululizo.
Baada ya kutolewa katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga ilirejea kwa kishindo kwa kuichapa Copco mabao 5-0 kwenye Kombe la Shirikisho. Kikosi cha kocha Sead Ramovic kimekuwa na kiwango bora katika mechi tano zilizopita za ligi, kikishinda zote huku kikifunga mabao 18 na kuruhusu mawili pekee.
Akizungumzia mchezo wa leo, Ramovic amesema kuwa Yanga imejiandaa kikamilifu na lengo ni kushinda kila mechi iliyosalia kwenye mzunguko wa pili. “Hautakuwa mchezo mwepesi kwa kuwa wapinzani wetu wanahitaji alama tatu, lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda ili kufanikisha malengo yetu ya kutetea ubingwa,” alisema Ramovic.
Kwa upande wa Kagera Sugar, mechi hii ni muhimu kwani timu hiyo ipo nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 11 pekee. Katika mechi tano zilizopita, imeambulia sare tatu na kupoteza mbili, hali inayoongeza presha ya kuhitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi salama. Kama Kagera Sugar itashinda leo, inaweza kupanda hadi nafasi ya 13 ikisubiri matokeo ya Tanzania Prisons.
Kocha wa Kagera Sugar, Mellis Medo, amekiri kuwa timu yake ipo kwenye wakati mgumu lakini ina mkakati wa kuzuia Yanga kufanikisha mashambulizi yao. “Hii ni mechi ngumu, tunacheza na timu yenye uzoefu mkubwa, lakini tutahakikisha tunawazuia kufanikisha mipango yao ya ushambuliaji na hatutaki kuwa wa kwanza kuruhusu bao,” alisema Medo.
Licha ya kuongeza nguvu kwenye usajili kwa kumsajili kipa Ahmed Feruzi, kiungo Mkenya Shaphan Siwa na mshambuliaji George Mpole, Kagera Sugar bado itamkosa Mpole kwenye mchezo wa leo kutokana na kutokamilisha taratibu za usajili kwa wakati.
Kikosi cha Yanga Vs Kagera Sugar Leo 01/02/2025
Kikosi rasmi cha Yanga Sc kitakacho anza leo dhidi ya Kagera Sugar kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa majira ya saa tisa jioni. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Yanga Sead Ramovic.
Nguvu ya Ushambuliaji ya Yanga na Presha kwa Kagera Sugar
Yanga itaingia dimbani ikiwa na safu kali ya ushambuliaji inayoongozwa na Clement Mzize mwenye mabao sita, Pacome Zouzoua pia mwenye mabao sita, na Prince Dube mwenye mabao matano. Jumla ya mabao yao matatu yanazidi mabao 10 ambayo Kagera Sugar imefunga katika mechi 15 za ligi hadi sasa.
Kwa upande wa rekodi, Kagera Sugar haijawahi kushinda dhidi ya Yanga katika mechi 10 zilizopita za Ligi Kuu. Katika kipindi hicho, Yanga imeshinda mechi nane huku mbili zikiishia kwa sare. Mchezo wa mwisho kati ya timu hizi ulimalizika kwa Yanga kushinda 2-0 huko Kaitaba, Bukoba.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Aliekua Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi Atua Al Nasr ya Libya
- Kagera Sugar Yatamba Kuondoa Unyonge KMC Complex Dhidi ya Yanga
- Morocco Aweka Mikakati ya Ushindi dhidi ya Vigogo Ndani ya Kundi C AFCON 2025
- Simba SC Yajiandaa Vikali Kuisambaratisha Tabora United
- Makundi ya Fainali za Mataifa ya Afrika AFCON 2025
- Tanzania Yapangwa Kundi C AFCON 2025
- Kundi la Taifa Stars AFCON 2025
- Timu zilizofuzu 32 bora CRDB Bank Federation Cup 2024/2025
Leave a Reply