Kikosi cha Simba SC vs CS Constantine Leo 19/01/2025

Simba SC vs CS Constantine Leo 19 01 2025

Kikosi cha Simba SC vs CS Constantine Leo 19/01/2025 | Kikosi cha Simba Leo Dhidi ya CS Constantine

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup), Simba SC, leo tarehe 19 Januari 2025 watashuka dimbani kuwakabili CS Constantine ya Algeria katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam. Mchezo huu wa hatua ya mwisho ya makundi unatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni, ukiwa wa muhimu kwa timu zote mbili katika kuamua nafasi ya mwisho ya msimamo wa Kundi A.

Simba SC, wakiwa na lengo la kulipa kisasi cha kipigo cha 2-1 walichokipata ugenini, wanahitaji ushindi wa lazima ili kumaliza kileleni mwa Kundi A. Ushindi huo utaifanya Simba kufikisha pointi 13 na kuizidi CS Constantine ambayo kwa sasa ina pointi 12. Kocha wa Simba, Fadlu Davids, amesisitiza kuwa timu yake itacheza kwa kujiamini huku wakilenga kumaliza hatua ya makundi wakiwa vinara.

“Tutacheza soka letu tulilozoea bila presha. Kumaliza kundi ukiwa wa kwanza ni muhimu kwa sababu hii itatuepusha kukutana na baadhi ya timu ngumu kama Zamalek na Al Masry kwenye hatua inayofuata,” alisema Davids.

Nyota wa Simba wakiongozwa na nahodha Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Jean Charles Ahoua wameeleza kuwa wana ari kubwa ya kuhakikisha ushindi wa leo unapatikana.

CS Constantine, ambao walishinda mchezo wa kwanza dhidi ya Simba kwa mabao 2-1, wanahitaji sare tu leo ili kulinda nafasi yao ya kuongoza kundi. Mchezo huo wa kwanza ulionyesha uimara wa Constantine, hasa walipopata mabao mawili katika kipindi cha pili kupitia Abdulrazack Hamza (bao la kujifunga) na Brahim Dib.

Simba, hata hivyo, wanajivunia rekodi nzuri ya nyumbani ambapo wamepata ushindi katika mechi zao zote za kimataifa msimu huu. Kocha Davids amewaonya wachezaji wake dhidi ya mbinu za kushtukiza za Constantine ambazo mara nyingi hutumika wanapokuwa ugenini.

Kikosi cha Simba SC vs CS Constantine Leo 19/01/2025

Kikosi cha Simba SC vs CS Constantine Leo 19/01/2025

Hiki apa ndicho kikosi cha Simba kitakachoanza leo dhidi ya CS Constantine

Kikosi cha Kwanza:

  1. Camara – Jezi namba 40
  2. Ngoma – Jezi namba 6
  3. Ahoua – Jezi namba 10
  4. Kapombe – Jezi namba 12
  5. Ateba – Jezi namba 13
  6. Hamza – Jezi namba 14
  7. Hussein (C) – Jezi namba 15
  8. Che Malone – Jezi namba 20
  9. Kagoma – Jezi namba 21
  10. Mpanzu – Jezi namba 34
  11. Kibu – Jezi namba 38

Wachezaji wa Akiba (Subs):

  1. Aishi
  2. Nouma
  3. Chamou
  4. Okejepha
  5. Mzamiru
  6. Fernandes
  7. Chasambi
  8. Mukwala
  9. Balua

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Yanga vs MC Alger Leo 18/01/2024 Saa Ngapi?
  2. Matokeo ya Yanga vs MC Alger Leo 18/01/2024
  3. Kikosi cha Yanga vs MC Alger Leo 18/01/2024
  4. Yanga Wamejipanga Kupambana Kesho: Ramovic
  5. Ligi Kuu Bara: JKT Tanzania Waitana Kambini, Kocha Apania Maboresho
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo