CECAFA Kagame Cup 2024: Michuano Ya Soka la Afrika Mashariki Larejea Tanzania! Hapa Tumekuletea Timu zitakazo shiriki CECAFA kagame cup 2024
Wakati michuano ya vilabu ndani ya nchi kuelekea tamati, sasa ni zamu ya mashabiki wa soka kushuhudia vilabu vyao pendwa vikipambana katika michuano mingine ya vilabu ngazi ya kimataifa.
Michuano ya Kagame CECAFA Cup ni moja kati ya mashindano yenye ushindani mkubwa na huambatana na mpira mzuri. Kama wewe ni shabiki wa mpira Afrika mashariki basi jiandae kwa kushuhudia michuano kabambe. Baada ya kusubiri kwa hamu kwa miaka miwili, CECAFA Kagame Cup inarejea kwa kishindo, na safari hii Tanzania ndio mwenyeji! Kuanzia tarehe 20 Julai hadi 4 Agosti, Dar es Salaam itakuwa uwanja wa vita vya soka, huku timu 16 bora kutoka kanda hii zikichuana vikali kuwania taji la klabu bingwa.
Timu zitakazo shiriki CECAFA kagame Cup 2024
Tayari majina makubwa yameanza kujitokeza! Yanga SC, wawakilishi wa Tanzania, watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya miamba kama vile Gor Mahia ya Kenya, Vital’O ya Burundi, SC Villa ya Uganda, na mabingwa watetezi APR ya Rwanda.
Lakini tusisahau timu nyingine 11 zitakazowakilisha mataifa yao kwa kujituma, zikiwemo zile kutoka mataifa ya Djibouti, Zanzibar, Sudan, Sudan Kusini, Ethiopia, Somalia, na Eritrea.
Na ili kuongeza msisimko zaidi, CECAFA imeahidi kualika timu 4 za ziada kutoka nje ya kanda, hivyo kufanya ushindani kuwa mkali zaidi!
CECAFA Kagame Cup sio tu mashindano ya soka, bali ni jukwaa la kuunganisha Afrika Mashariki kupitia mchezo huu pendwa. Ni fursa kwa wachezaji wetu kuonyesha vipaji vyao, kwa mashabiki kujumuika pamoja, na kwa mataifa yetu kuimarisha uhusiano.
Timu zilizofuzu kucheza michuano ya CECAFA Kagame Cup inayotarajiwa kuanzia Julai 20 hadi Agosti 4, 2024
- Vital ‘0 (Burundi)
- APR FC (Rwanda)
- El Merreikh (Sudan)
- Al Hilal (Sudan)
- Hai El Wadi (Sudan)
- Young Africans SC (Tanzania)
- Simba SC (Tanzania)
- Azam FC (Tanzania)
- Coastal Union FC (Tanzania)
- Gor Mahia FC (Kenya)
- SC Villa (Uganda)
- JKU SC (Zanzibar)
- El Merreikh FC-Bentiu (South Sudan)
- Nyasa Big Bullets FC (Malawi)
- TP Mazembe (DR Congo)
- Red Arrows FC (Zambia).
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply