Matokeo ya Bravos do Maquis vs Simba SC Leo 12/01/2025 | Matokeo ya Simba Leo Dhidi ya Bravos Kombe la Shirikisho
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, leo wanakabiliwa na kibarua kigumu cha kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika. Saa 1:00 usiku, macho ya mashabiki wa soka Tanzania yataelekezwa Uwanja wa Novemba 11, Luanda, Angola, ambapo Simba watavaana na wenyeji wao Bravos do Maquis.
Hii ni mechi ya raundi ya tano ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF, na Simba wanahitaji ushindi au sare ili kujihakikishia nafasi katika robo fainali kutoka Kundi A. Je, Wekundu wa Msimbazi wataweza kuhimili vishindo vya Bravos do Maquis ugenini?
Simba imewasili Angola ikiwa na lengo moja tu: Kushinda. Kocha Fadlu Davids anajua fika umuhimu wa mchezo huu katika Uwanja wa 11 de Novembro. Ushindi utawapunguzia presha katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Constantine.
Katika msimamo wa Kundi A, Simba wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi tisa, sawa na vinara CS Constantine. Bravos do Maquis wako nafasi ya tatu na pointi sita, huku CS Sfaxien wakiburuza mkia bila pointi.
Endapo Constantine wataifunga Sfaxien leo, watafuzu robo fainali moja kwa moja. Hivyo basi, Simba hawana budi kupata ushindi au sare dhidi ya Bravos ili kujihakikishia nafasi.
Rekodi zinaonyesha kwamba Simba na Bravos zote hutegemea sana kipindi cha kwanza kupata matokeo. Simba imefunga mabao manane katika mechi sita, na sita kati ya hayo yamepatikana kipindi cha kwanza.
Nguvu ya Simba ipo katika safu yao ya kiungo, inayoongozwa na Kibu Denis mwenye mabao matatu na Jean Charles Ahoua mwenye mabao mawili. Ahoua amekuwa mchezaji muhimu kwa Simba, akiwa kinara wa kutengeneza nafasi katika kikosi hicho.
Bravos nao wamekuwa wakitumia vyema kipindi cha kwanza kupata mabao. Kati ya mabao 12 waliyofunga, saba yamepatikana katika kipindi cha kwanza. Wachezaji hatari wa Bravos ni Jo Paciencia na Francisco Cabuema Matoco “Macaiabo”, kila mmoja akiwa na mabao matatu. Kocha wa Bravos, Mario Soares, ametambua ubora wa Ahoua na kumtaja kama mchezaji hatari zaidi katika kikosi cha Simba. Hata hivyo, Soares anaamini kuwa Bravos watapambana kupata ushindi nyumbani.
Matokeo ya Bravos do Maquis vs Simba SC Leo 12/01/2025
Bravos do Maquis | VS | Simba Sc |
- Michuano: TotalEnergies CAF Confederation Cup (Raundi ya Tano – Hatua ya Makundi)
- Timu: Bravos do Maquis vs Simba SC
- Tarehe: Jumapili, 12 Januari 2025
- Uwanja: Uwanja wa Novemba 11, Luanda, Angola
- Muda: Saa 1:00 usiku (Tanzania)
Waamuzi wa Mchezo Wa Bravos do Maquis vs Simba SC Leo
Mwamuzi Jean Ouattara kutoka Burkina Faso ndiye atakayepuliza kipenga katika mchezo huu. Ouattara ni mwamuzi mwenye uzoefu katika mechi za CAF, na anatarajiwa kuchezesha kwa haki.
Mavambo Arejea Nyumbani
Kiungo wa Simba, Debora Mavambo, anatarajiwa kuwa kivutio kikubwa katika mchezo huu. Mavambo, ambaye ni mzaliwa wa Angola, amewahi kucheza soka nchini humo kabla ya kujiunga na Simba akitokea Zambia.
Mavambo anajua fika ugumu wa kucheza dhidi ya Bravos nyumbani, lakini anaamini Simba ina uwezo wa kupata matokeo mazuri.
Je, Nyavu Zitatikisika?
Bravos hawajawahi kupoteza mchezo nyumbani katika michuano ya CAF msimu huu, na wamekuwa wakifunga mabao katika kila mchezo. Simba nao wamekuwa wakifunga mabao katika mechi zao za ugenini. Hivyo basi, kuna uwezekano mkubwa wa kushuhudia mabao katika mchezo huu.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi cha Yanga VS Al Hilal Leo 12/01/2025
- Bravos do Maquis vs Simba SC Leo 12/01/2025 Saa Ngapi?
- Ratiba ya Mechi za Leo 12/01/2025
- Al Hilal VS Yanga Leo 12/01/2025 Saa Ngapi?
- Timu Zilizofuzu Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
- Rachid Taoussi Apania Kushusha Nyota Zaidi Dirisha Dogo
- AS Vita Yamnyakua Dennis Modzaka Kutoka Coastal Union
- Walioitwa Kwenye Usaili Uhamiaji 2025
- Rabbin Sanga Ajiunga na Tanzania Prisons Kwa Mkopo
- Robert Matano Ateuliwa Kuwa Kocha Mkuu wa Fountain Gate FC
- Msimamo wa Kundi la Yanga Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025
- Mazembe Yaondolewa Ligi ya Mabingwa na MC Alger Baada ya Kipigo cha 1-0
- Bao la Inzaghi Laipa Zanzibar Heroes Tiketi ya Fainali Kombe la Mapinduzi
Leave a Reply