Bao la Inzaghi Laipa Zanzibar Heroes Tiketi ya Fainali Kombe la Mapinduzi
Zanzibar Heroes wamefanikiwa kufuzu kwa fainali ya Kombe la Mapinduzi 2025 baada ya kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Harambee Stars kutoka Kenya. Mchezo huu wa kusisimua ulifanyika Januari 10, 2025, kwenye Uwanja wa Gombani, kisiwani Pemba.
Bao la pekee lililowawezesha wenyeji kuendelea na michuano lilifungwa na Ali Khatib ‘Inzaghi’ dakika ya 90+4, akimalizia kwa kichwa kona iliyopigwa na nahodha, Feisal Salum ‘Fei Toto’.
Kenya, ambayo ilihitaji sare ili kufikia pointi tano na kupiga hatua kwenda fainali, ilijaribu kutumia mbinu ya kupoteza muda katika dakika za mwisho za mchezo. Licha ya jitihada hizo, walikosa bao la kusawazisha na walikubali kipigo cha 1-0 kutoka kwa Zanzibar Heroes. Matokeo haya yamewafanya Harambee Stars kumaliza na pointi nne, wakikosa nafasi ya kutinga fainali.
Katika mchezo huo, wachezaji wawili walionyeshwa kadi nyekundu. Kadi ya kwanza ilitolewa kwa nahodha wa Kenya, Abdu Omar, dakika ya 68 baada ya kugomea kutii adhabu ya kadi hiyo. Alihitaji muda mrefu kutoka uwanjani, ambapo alihitaji kujadiliana na Fei Toto pamoja na wachezaji wenzake kabla ya kuondoka. Dakika ya 90+9, beki wa Zanzibar Heroes, Ibrahim Ame, naye alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumalizika kwa mchezo.
Kwa ushindi huu, Zanzibar Heroes wamefikisha pointi sita na kumaliza nafasi ya pili kwenye kundi lao, nyuma ya Burkina Faso iliyo na pointi saba. Wakati huo, Kenya ilimaliza na pointi nne, huku Kilimanjaro Stars ikimaliza bila pointi yoyote baada ya kushindwa katika mechi zote tatu.
Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2025 itachezwa Januari 13, 2025, kwenye Uwanja wa Gombani, ambapo Zanzibar Heroes itakutana na Burkina Faso. Timu hiyo ya Burkina Faso ilifuzu kwa fainali baada ya kuichapa Kilimanjaro Stars 2-0 na kufikisha pointi saba.
Tuzo ya Mshindi wa Kombe la Mapinduzi 2025
Bingwa wa Kombe la Mapinduzi 2025 atapata kitita cha shilingi milioni 100. Mashabiki wanatarajia kushuhudia mchezo wa kipekee kati ya Zanzibar Heroes na Burkina Faso huku fainali hii ikileta ushindani mkali na furaha kwa wapenzi wa soka.
Mapendekezo ya Mhariri:
- CV ya Jonathan Djogo Kapela: Winga Mpya wa Yanga SC
- Zouzou Landry Atua Azam FC Kutoka Ivory Coast
- Kilimanjaro Stars Yaondolewa Mapinduzi Cup Bila Bao Wala Pointi
- Matokeo ya Tanzania Bara vs Burkina Faso Leo 09/01/2025
- Kikosi cha Simba Kilicho Safiri Kwenda Angola Kuifuata Bravos
- Shassir Nahimana (31) Atambulishwa Rasmi na Pamba Jiji
- Kilimanjaro Stars Kukamilisha Ratiba Mapinduzi Cup Dhidi ya Burkina Faso
- Msimamo Wa Kundi Mapinduzi Cup 2025
- Kikosi cha Kilimanjaro Stars vs Kenya Leo 07/01/2025
- Msimamo wa Kundi la Yanga Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025
Leave a Reply