Matokeo ya Tanzania Bara vs Burkina Faso Leo 09/01/2025

Tanzania Bara vs Burkina Faso Leo Saa Ngapi

Matokeo ya Tanzania Bara vs Burkina Faso Leo 09/01/2025 | Matokeo ya Kilimanjaro Star Leo Dhidi ya Burkina Faso

TIMU ya Soka ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) inakutana na Burkina Faso leo tarehe 09 Januari 2025 katika mechi ya kukamilisha ratiba ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi. Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Gombani, kisiwani Pemba, ikiwa ni sehemu ya hatua za awali za mashindano hayo yanayoshirikisha timu za taifa mwaka huu.

Kilimanjaro Stars tayari imejiondoa kwenye mashindano baada ya kushindwa kufurukuta katika mechi mbili zilizopita. Timu hiyo, inayonolewa na Kocha Mkuu Hamad Ally, ilianza kwa kupoteza dhidi ya Zanzibar Heroes kwa bao 1-0 katika mechi ya ufunguzi. Matarajio ya kurejea kwenye ushindani yalizimwa baada ya kufungwa mabao 2-0 na Kenya katika mechi iliyochezwa juzi usiku.

Mashindano ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu yanaonyesha ushindani mkubwa kati ya timu zinazoshiriki. Kwa mujibu wa msimamo wa kundi, Kenya na Burkina Faso zinaongoza kwa pointi nne kila moja, huku Zanzibar Heroes wakiwa nafasi ya tatu na pointi tatu. Tanzania Bara, bila pointi, iko nafasi ya mwisho katika kundi hilo.

Mechi ya leo ni muhimu kwa Burkina Faso, ambayo ina nafasi ya kuimarisha nafasi yake kileleni kwa kushinda. Hii pia ni fursa kwa Zanzibar Heroes, ambao watakutana na Burkina Faso katika mechi nyingine ya leo, kujaribu kufuzu kwa hatua ya fainali.

Matokeo ya Tanzania Bara vs Burkina Faso Leo 09/01/2025

Matokeo ya Tanzania Bara vs Burkina Faso Leo 09/01/2025

Tanzania Bara 0-2 Burkina Faso

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Simba Kilicho Safiri Kwenda Angola Kuifuata Bravos
  2. Tanzania Bara vs Burkina Faso Leo 09/01/2025 Saa Ngapi?
  3. Kilimanjaro Stars Kukamilisha Ratiba Mapinduzi Cup Dhidi ya Burkina Faso
  4. Shassir Nahimana (31) Atambulishwa Rasmi na Pamba Jiji
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo