Kikosi cha Kilimanjaro Stars vs Kenya Leo 07/01/2025 | Kikosi cha Tanzania Vs Kenya Leo Mapinduzi Cup
BAADA ya jana Jumatatu michuano ya Kombe la Mapinduzi 2025 kuendelea kwa mzunguko mwingine baada ya Januari 3 na 4 kupigwa mechi mbili, leo ni zamu ya Kilimanjaro Stars dhidi ya Kenya kujiuliza. Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa kusisimua na muhimu sana kwa timu zote mbili.
Mchezo huu wa kihistoria utaanza saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Gombani uliopo Kisiwani Pemba. Ni mechi ambayo inatazamiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi kutokana na umuhimu wake katika kuamua hatima ya timu zitakazopata nafasi ya kucheza fainali ya michuano hii maarufu.
Kilimanjaro Stars, ambayo inawakilisha Tanzania Bara, ilianza michuano hii kwa matokeo yasiyoridhisha baada ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Zanzibar Heroes. Hali hii imeiweka katika nafasi ngumu ambapo wanapaswa kushinda mchezo wa leo ili kufufua matumaini yao ya kusonga mbele. Kwa upande mwingine, Kenya ilianza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Burkina Faso, na hivyo kujiweka katika nafasi bora zaidi kuliko wapinzani wao.
Katika msimamo wa michuano hii kabla ya mchezo wa jana kati ya Zanzibar Heroes na Burkina Faso, Zanzibar Heroes walikuwa vinara wakiwa na pointi tatu, wakifuatiwa na Burkina Faso na Kenya ambao wote walikuwa na pointi moja kila mmoja, huku Kilimanjaro Stars wakiwa hawana alama.
Kikosi cha Kilimanjaro Stars vs Kenya Leo 07/01/2025
Kikosi rasmi cha Kilimanjaro Stars kitakacho anza leo dhidi ya Kenya kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 12 jioni. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Kilimanjaro Stars Ahmad Aally.
Kauli za Makocha
Kocha wa Kilimanjaro Stars, Ahmad Ally, amesisitiza kuwa mchezo huu hautakuwa rahisi lakini wamejipanga vyema kuhakikisha wanapata ushindi muhimu. “Hautakuwa mchezo rahisi kutokana na wapinzani wetu tulivyowaona walivyocheza mechi yao, hivyo tunahitaji kujitoa kwa asilimia mia mchezo wa kesho (leo) tupate ushindi,” alisema Kocha Ally. Ameongeza kuwa wameangalia mbinu zote za wapinzani wao ili kuhakikisha wanadhibiti mchezo na kufanikisha malengo yao.
Kwa upande wake, Kocha wa Kenya, Fransi Kimanzi, amesema kuwa timu yake imejiandaa vyema na ana imani kubwa kwamba watatoa burudani ya hali ya juu kwa mashabiki. “Tumeendelea kujiandaa kufanya vizuri, tunaamini mchezo wa kesho (leo) utakuwa mzuri na kuwaburudisha mashabiki,” alisema Kocha Kimanzi.
Mustakabali wa Michuano
Baada ya mchezo wa leo, michuano hii itapumzika kesho Jumatano kabla ya kuendelea tena Januari 9 ambapo Kilimanjaro Stars watakutana na Burkina Faso. Zanzibar Heroes nao watachuana na Kenya Januari 10. Timu mbili zitakazokuwa na pointi nyingi baada ya mechi hizi zitatinga fainali itakayochezwa Januari 13.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kilimanjaro Stars vs Kenya Leo 07/01/2025 Saa Ngapi?
- Msimamo wa Kundi la Yanga Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025
- Kikosi cha Simba SC vs CS Sfaxien Leo 05/01/2024
- CS Sfaxien vs Simba SC Leo 05/01/2024 Saa Ngapi?
- Kikosi cha Yanga vs Tp Mazembe Leo 04/01/2024
- Yanga Kuwakosa Maxi, Chama na Yao Mechi Dhidi ya TP Mazembe Leo
Leave a Reply