Matokeo ya Yanga vs Tanzania Prison leo 22/12/2024 | Matokeo ya Yanga leo dhidi ya Tz Prison
Leo ni siku nyingine muhimu kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, ambao leo watashuka dimbani kukabiliana na Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu unaotarajiwa kuwa wenye ushindani mkubwa.
Mechi hii itachezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam, kuanzia saa 10:00 jioni. Yanga watalenga kuimarisha nafasi yao kwenye msimamo wa ligi, huku Tanzania Prisons wakipigania kujiondoa katika eneo hatarishi la kushuka daraja.
Yanga SC inashuka dimbani ikiwa na morali ya ushindi kutoka mchezo uliopita dhidi ya Mashujaa, ambapo walishinda kwa mabao 3-2, huku Prince Dube akitengeneza historia kwa kupiga hat trick ya kwanza msimu huu. Ushindi huo ulionyesha mabadiliko makubwa katika kiwango cha timu, huku pasi sahihi na mashambulizi ya kasi vikichukua nafasi kubwa kwenye mchezo huo.
Licha ya mafanikio hayo, Yanga bado inakabiliwa na changamoto za majeruhi kwa wachezaji wao muhimu kama kipa Djigui Diarra na viungo Maxi Nzengeli na Clatous Chama. Hata hivyo, ujio wa Kibwana Shomari ulileta nguvu mpya kwenye safu ya ushambuliaji, huku akiweka rekodi ya kutoa asisti muhimu kwenye ushindi wa mchezo uliopita.
Yanga kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 30 baada ya michezo 13, huku ikisalia na viporo viwili. Lengo lao ni kuhakikisha wanashinda michezo yote iliyobaki ili kufikisha alama 39 kabla ya kuanza kwa duru ya pili.
Kwa upande wa Tanzania Prisons inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na hali ngumu baada ya kushinda mechi mbili tu kati ya 14 walizocheza hadi sasa. Timu hiyo inashikilia nafasi ya pili kutoka chini, ikiwa na alama 11 pekee. Changamoto kubwa kwa Prisons ni ukosefu wa mshambuliaji wa kutegemewa, kwani mabao yao sita yamefungwa na wachezaji tofauti bila mchezaji yeyote kufikisha zaidi ya bao moja.
Hata hivyo, kuingia kwa Kaimu Kocha Mkuu Shaban Mtupa kunaleta matumaini mapya. Mtupa amesema timu yake imekuwa ikifanyia kazi maeneo yenye upungufu na kuimarisha morali ya wachezaji. Ingawa wanakutana na Yanga, timu yenye rekodi bora dhidi yao, Prisons inatarajia kupambana kwa nguvu kuhakikisha wanapata matokeo chanya.
Matokeo ya Yanga vs Tanzania Prison leo 22/12/2024
Yanga Sc | 4-0 | Tz Prison |
- 🏆 #NBCPremierLeague
- ⚽️ Young Africans SC🆚TZ Prisons
- 📆 22.12.2024
- 🏟 KMC Complex
- 🕖 10:00 Jioni
Rekodi za Hapo Awali
Takwimu zinaonyesha kwamba Yanga imekuwa ikitawala michezo yao dhidi ya Prisons. Katika mechi 24 zilizopita tangu msimu wa 2012/2013, Yanga imeshinda michezo 16 na kutoka sare mara 8, bila kupoteza mchezo wowote. Rekodi hii inaweka wazi changamoto inayowakabili Prisons, ambao wameshindwa kupata ushindi kwenye michezo mitano ya mwisho dhidi ya Yanga.
Wachezaji wa Kuzingatiwa
- Prince Dube (Yanga SC): Baada ya kupiga hat trick kwenye mchezo uliopita, Dube anaonekana kuwa kwenye kiwango bora na anatarajiwa kuendeleza kasi yake ya kufumania nyavu.
- Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli (Yanga SC): Ingawa Maxi anauguza majeraha, ushirikiano wake na Zouzoua umeendelea kuwa muhimu kwa safu ya ushambuliaji wa Yanga.
- Meshack Abraham (Tanzania Prisons): Mchezaji huyu wa Prisons ni mmoja wa wachezaji walioweka alama msimu huu, na mchango wake unaweza kuwa muhimu kwa timu yake katika mchezo huu.
Kauli za Makocha
Kocha Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic, amesema: “Tunahitaji kuzingatia kila sekunde kwenye mchezo huu. Heshima kwa wapinzani wetu ni jambo muhimu, lakini lengo letu ni kushinda na kuongeza pointi tatu.”
Kwa upande wa Kaimu Kocha Mkuu wa Prisons, Shaban Mtupa, amesema: “Licha ya changamoto, tuna imani na wachezaji wetu. Tunahitaji kujihadhari na makosa madogo na kutumia nafasi tunazopata ipasavyo.”
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi cha Yanga vs Tanzania Prison leo 22/12/2024
- Vita ya Kumsajili Okoyo Yazuka Kati ya KMC, Mashujaa na Namungo
- Guede Afunguka Sababu za Kutemwa Singida Black Stars
- Kagera Sugar Karibu Kumsajili Adam Adam Kutoka Azam FC
- Banda Avunja Mkataba na Baroka FC Baada ya Miezi 3 Tu
- Winga wa Zamani wa Simba Yusuph Mhilu Atamani Kurejea Ligi Kuu
Leave a Reply