Dube Afunga Goli 3 na Kuipa Yanga Ushindi Dhidi ya Mashujaa
Baada ya mateso, vilio, na manung’uniko, hatimaye Mungu amejibu maombi ya mshambuliaji wa Yanga, Prince Mpumelelo Dube. Katika mchezo uliovuta hisia za mashabiki wengi wa soka hasa wa Yanga Sc, Dube alionesha umahiri wake baada ya kufunga magoli yote matatu (hattrick) kwenye ushindi muhimu wa 3-2 walioupata Wananchi dhidi ya Mashujaa FC kwenye dimba la KMC Complex.
Kabla ya mchezo huu, Dube alikuwa hajafunga bao lolote kwenye Ligi Kuu msimu huu, lakini upepo umebadilika na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza msimu huu kufanikisha hat-trick.
Muhtasari wa Mchezo
Mchezo ulianza kwa kasi huku Yanga ikionekana kuwa na shauku ya kurejesha ushindi baada ya matokeo ya kusuasua kwenye mechi za hivi karibuni. Prince Dube aliwaweka Wananchi kifua mbele mapema dakika ya 7 kwa goli la kwanza, akionyesha umahiri wake wa kumalizia nafasi mbele ya lango. Aliongeza bao la pili dakika ya 21, ambalo liliimarisha uongozi wa Yanga.
Hata hivyo, Mashujaa FC hawakukata tamaa. Dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza, Oromi aliipatia Mashujaa goli muhimu lililorejesha matumaini kwa timu hiyo. Baada ya mapumziko, Yanga walirejea kwa ari mpya, na Dube alikamilisha hat-trick yake dakika ya 53 kwa shuti kali lililomshinda kipa wa Mashujaa.
Mashujaa walipunguza tena tofauti dakika ya 62 kupitia goli la Idrisa Stambuli, lakini juhudi zao za kusawazisha hazikufua dafu. Yanga waliendelea kudhibiti mchezo hadi kipenga cha mwisho, wakihakikisha pointi zote tatu zinabaki mikononi mwao.
Maana ya Ushindi kwa Yanga
Ushindi huu umeipeleka Yanga SC hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, wakiwa na jumla ya pointi 30 baada ya michezo 12. Wananchi sasa wako pointi moja tu nyuma ya mahasimu wao, Simba SC, waliopo nafasi ya pili. Hii inatoa matumaini makubwa kwa mashabiki wa Yanga kuhusu harakati za kutetea ubingwa wao msimu huu.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Hiki Apa Kikosi cha Yanga Vs Mashujaa Leo 15/12/2024
- Matokeo ya Yanga vs Mashujaa leo 19/12/2024
- Washindi wa Tuzo za CAF 2024 (CAF AWARDS 2024)
- Msimamo Kundi la Simba Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025
- Kibu Denis Aipa Simba Ushindi Dhidi ya CS Sfaxien Dakika za Jioni
- Matokeo ya Simba VS CS Sfaxien Leo 15/12/2024
- Jackson Shiga Anukia Fountain Gate
Leave a Reply