Yanga Yapasuka Tena Klabu Bingwa, Yachapwa 2-0 na MC Alger
Mambo yanazidi kuwa magumu kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania, Yanga SC, katika michuano ya kimataifa ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kuchezea kichapo cha chuma 2-0 dhidi ya wenyeji wao MC Alger katika mchezo uliochezeka kwenye dimba la 5 July 1962. Hii ni mechi ya pili mfululizo ambayo Yanga SC inapoteza baada ya ile ya nyumbani dhidi ya Al Hilal, ambayo ilimalizika kwa timu ya Wananchi kula chuma 2-0 mbele ya maelfu ya mashabiki wao waliojitokeza uwanjani.
Katika mchezo huu ambao mashabiki wengi wa soka Tanzania walitegemea kuona Yanga wakionesha ubora wa hali ya juu, MC Alger walitumia vyema fursa yao ya kua nyumbani kuhakikisha wanapata alama zote tatu muhimu. Bao la kwanza lilifungwa na Abdellaoui dakika ya 64 kupitia mpira wa kona uliosababisha mkanganyiko kwenye safu ya ulinzi ya Yanga. Bao la pili, ambalo lilikuwa kama msumari wa mwisho kwa Yanga, lilifungwa na Bayazid katika dakika ya 90+5, likihitimisha matumaini yoyote ya Wananchi kurejea mchezoni.
Yanga SC sasa wanaburuza mkia katika msimamo wa Kundi A wakiwa hawajakusanya alama yoyote baada ya mechi mbili.
Matokeo haya yanaweka shinikizo kubwa kwa kocha wao pamoja na wachezaji, ambao wanatakiwa kupambana vilivyo katika michezo iliyosalia ili kufufua matumaini yao ya kusonga mbele kwenye hatua ya mtoano.
Kundi A linaonekana kuwa changamoto kubwa kwa Yanga, huku MC Alger wakipanda kileleni wakiwa na alama 4, wakifuatiwa na timu nyingine ambazo nazo zinaonyesha ushindani mkubwa.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Matokeo ya MC Alger VS Yanga SC Leo 7/12/2024
- Kikosi cha Yanga SC vs MC Alger Leo 7/12/2024
- Ushindi wa Namungo dhidi ya Tanesco Wampa Mgunda Tumaini
- Hizi Apa Mbinu Za Fadlu Za Kuisambaratisha CS Constantine
- MC Alger Vs Yanga Leo 07/12/2024 Saa ngapi?
- Makundi ya Kombe la Dunia la Vilabu 2025
- Kikosi cha Yanga Tayari kwa Vita ya Algiers
Leave a Reply