Makundi ya Kombe la Dunia la Vilabu 2025
Droo ya mashindano mapya ya Kombe la Dunia kwa ngazi ya klabu ilifanyika Desemba 5, 2024, saa 3:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, Marekani. Mashindano haya yaliyosubiriwa kwa hamu yatashirikisha jumla ya timu 32 zilizogawanywa katika makundi nane ya timu nne kila moja. Tofauti na miaka ya nyuma ambapo Kombe la Dunia la Vilabu lilishirikisha timu saba tu.
Mashindano haya sasa yatafanyika kila baada ya miaka minne yakihusisha timu zilizofanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya Klabu Bingwa ya mabara sita (AFC, CAF, Concacaf, Conmebol, OFC, na UEFA) katika kipindi cha misimu minne iliyopita. Bara la Ulaya limepewa nafasi kubwa kwa kutoa timu 12, wakati Afrika, Asia, na Amerika ya Kaskazini kila moja itatoa timu nne. Amerika ya Kusini itawakilishwa na timu sita, huku Bara la Oceania likiwa na mwakilishi mmoja.
Mashindano haya yataanza rasmi Juni 15, 2025, na kufikia kilele chake Julai 13, 2025, ambapo mchezo wa fainali utaamua bingwa wa dunia kwa ngazi ya vilabu. Kila timu itacheza dhidi ya nyingine kwenye kundi lake, huku timu mbili bora kutoka kila kundi zikifuzu hatua ya mtoano.
Timu Zilizofuzu na Muundo wa Mashindano
Timu zitakazoshiriki mashindano haya ni zile ambazo zimeshinda au kufanya vyema katika michuano ya Klabu Bingwa kutoka kwa misimu minne iliyopita kutoka mabara mbalimbali.
Bara la Ulaya (UEFA) litaongoza kwa kutoa timu 12, huku Bara la Afrika (CAF), Asia (AFC), na Amerika ya Kaskazini (CONCACAF) zikitatoa timu nne kila moja. Amerika ya Kusini (CONMEBOL) itatoa timu sita, na bara la Oceania (OFC) litatoa timu moja pekee.
Kila kundi litajumuisha timu nne, na kila timu itacheza mechi moja dhidi ya timu nyingine kwenye kundi lake. Timu mbili bora kutoka kila kundi zitafuzu kwa hatua ya mtoano, ambapo hakutakuwa na mchezo wa kuwania nafasi ya tatu. Mchezo wa fainali utachezwa Julai 13, 2025, na ushindi wa kombe hili unatarajiwa kuwa tukio kubwa la kihistoria katika soka la kimataifa.
Makundi ya Kombe la Dunia la Vilabu 2025
- Kundi A: Palmeiras, Al Ahly, Porto, Inter Miami
- Kundi B: Paris Saint-Germain, Atletico Madrid, Botafogo, Seattle Sounders
- Kundi C: Bayern Munich, Auckland City, Boca Juniors, Benfica
- Kundi D: Flamengo, Esperance Sportive de Tunisie, Chelsea, León
- Kundi E: River Plate, Urawa Red Diamonds, Monterrey, Inter Milan
- Kundi F: Fluminense, Borussia Dortmund, Ulsan, Al Hilal
- Kundi G: Manchester City, Wydad Casablanca, Juventus
- Kundi H: Real Madrid, Al Hilal, Pachuca, Salzburg
Mapendekezo ya Mhariri:
- Matokeo ya MC Alger VS Yanga SC Leo 7/12/2024
- Kikosi cha Yanga SC vs MC Alger Leo 7/12/2024
- MC Alger Vs Yanga Leo 07/12/2024 Saa ngapi?
- Kikosi cha Yanga Tayari kwa Vita ya Algiers
- Fei Toto Aendelea Kuwaka Ligi Kuu, Anaongoza kwa Mabao na Assists
- Coastal waweka wazi mpango wa kutinga Nne bora Ligi Kuu
Leave a Reply