Matokeo ya MC Alger VS Yanga SC Leo 7/12/2024 | Matokeo ya Yanga leo dhidi ya MC Alger Klabu Bingwa
Yanga SC, mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania, wanatarajiwa kushika dimbani kucheza mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika leo Desemba 7, 2024, dhidi ya MC Alger katika uwanja wa kihistoria wa Julai 5, 1962.
Mchezo huu unakuwa muhimu kwa Yanga ambao wameanza hatua ya mkakundi kwa kichapo nyumbani, ikizingatiwa rekodi za wapinzani wao kwenye michezo ya nyumbani hazijajaa mafanikio. Takwimu za MC Alger zinaonesha udhaifu wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani, jambo linalotoa matumaini makubwa kwa Yanga kupata matokeo chanya.
Matokeo ya MC Alger VS Yanga SC Leo 7/12/2024
MC Alger | 2-0FT | Yanga Sc |
- 🏆 #CAFCL
- ⚽️ MC Alger🆚Young Africans SC
- 📆 07.12.2024
- 🏟 5 July 1962
- 🕖 8pm🇩🇿 10pm🇹🇿
Fuatilia hapa Kikosi cha Yanga SC vs MC Alger Leo 7/12/2024
Rekodi ya MC Alger Kwenye Ligi ya Ndani
Katika michezo 10 ya Ligi Kuu ya Algeria msimu huu, MC Alger imefanikiwa kushinda mechi nne pekee, kutoka sare tano, na kupoteza mchezo mmoja. Kwa michezo ya nyumbani, wamecheza mara tano, wakishinda mara moja tu, kutoka sare tatu, na kufungwa mara moja. Wamevuna alama sita kati ya 15 zinazowezekana, hali inayoashiria changamoto kubwa ya kuonyesha uimara wakiwa nyumbani.
Hali ni tofauti kidogo wanapocheza ugenini, ambapo MC Alger imepata ushindi mara tatu na kutoka sare mbili katika michezo mitano, ikivuna alama 11 kati ya 15. Hii inathibitisha kuwa wamekuwa bora zaidi wakiwa ugenini kuliko wanapokuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.
Mchezo wa pekee waliopata ushindi nyumbani msimu huu walipoifunga El Bayadh kwa bao 1-0, timu inayoshikilia nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu Algeria. Katika michezo mingine, walikubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa CR Belouizdad, mabingwa wa zamani wa Algeria.
Nguvu ya Kikosi cha Yanga SC
Yanga SC wamesafiri wakiwa na kikosi chao kamili chenye nyota kama Stephan Aziz Ki, Pacome Zouzoua, Max Nzengeli, Ibrahim Bacca, na Djigui Diarra. Kikosi hiki kina nguvu na uzoefu mkubwa wa kimataifa, hasa baada ya mafanikio yao ya msimu uliopita katika ligi ya ndani na mashindano ya Afrika.
Nyota hawa wakiwa na maelewano mazuri uwanjani, wana nafasi nzuri ya kutumia udhaifu wa MC Alger na kuhakikisha wanaondoka na alama tatu muhimu. Uwepo wa wachezaji wenye uzoefu wa kupambana na timu za Kiarabu, kama ilivyoonekana katika ushindi wao wa awali dhidi ya USM Alger na Club Africain, kunawapa Yanga SC nafasi kubwa ya kushinda.
Mapendekezo ya Mhariri:
- MC Alger Vs Yanga Leo 07/12/2024 Saa ngapi?
- Kikosi cha Yanga Tayari kwa Vita ya Algiers
- Fei Toto Aendelea Kuwaka Ligi Kuu, Anaongoza kwa Mabao na Assists
- Coastal waweka wazi mpango wa kutinga Nne bora Ligi Kuu
- Chikola Atwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Novemba
- Ratiba ya Simba Sc December 2024
- Ratiba ya Yanga Sc December 2024
Leave a Reply