Fei Toto Aendelea Kuwaka Ligi Kuu, Anaongoza kwa Mabao na Assists
Kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’, anaendelea kufanya vyema katika Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo mpaka sasa amethibitisha ubora wake kwa kuongoza kwa idadi kubwa ya mabao na pasi za mwisho. Fei Toto amekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa soka nchini, kutokana na umiliki wake mzuri wa mpira, ustadi wake wa kufunga mabao, na mchango wake mkubwa katika kutoa pasi nzuri za mwisho (Assist) kwa wachezaji wenzake.
Hadi kufikia raundi ya 13 ya Ligi Kuu, Fei Toto ameonyesha kiwango cha juu kwa kufunga mabao manne, ambapo matatu kati ya hayo ameyapata kwa njia ya penalti. Hii inamfanya kuwa kinara katika orodha ya wachezaji waliofunga mabao mengi ya penalti. Mchezo mmoja muhimu ambao ulionyesha ufanisi wake ni ule dhidi ya KenGold, ambapo Fei Toto alifunga mabao matatu ya penalti, na hivyo kutoa mchango mkubwa katika ushindi wa 4-1 wa Azam FC.
Katika mchezo mwingine dhidi ya Kagera Sugar, Fei Toto alifunga bao la pekee ambalo lilisaidia Azam kushinda 1-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex. Hii ni ishara ya uwezo wake wa kutengeneza nafasi na kuzitumia vizuri, akiendelea kuonyesha umahiri katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mabao ya Penalti na Wachezaji Wanaomfukuzia Feisal
Ingawa Fei Toto ameongoza kwa kufunga penalti tatu, bado ana ushindani mkubwa kutoka kwa wachezaji wengine katika Ligi Kuu. Jean Ahoua na Leonel Ateba wameshika nafasi ya pili kwa kufunga mabao mawili kila mmoja kwa njia ya penalti. Ahoua alifunga mabao yake ya penalti kwenye michezo dhidi ya Dodoma Jiji na KMC, huku Ateba akifunga katika michezo dhidi ya Coastal Union na Pamba Jiji. Ogochukwu Morice wa Tabora United pia alifunga mabao mawili ya penalti, akifanya hivyo dhidi ya Pamba Jiji na Mashujaa.
Fei Toto Aongoza kwa Asisti
Mbali na mabao, Fei Toto pia anaongoza kwa kutoa asisti nyingi katika Ligi Kuu Tanzania Bara. Hadi sasa, ameweza kutoa asisti tano, akiongoza orodha ya wachezaji waliochangia mabao kwa njia ya pasi. Wachezaji wengine wanaofuatia kwa kutoa asisti nyingi ni Jean Ahoua wa Simba na Salum Kihimbwa wa Fountain Gate, ambao kila mmoja ametoa asisti nne. Hii inaonesha kuwa Fei Toto ni mchezaji ambaye siyo tu anajua kufunga, bali pia anajua jinsi ya kumsaidia mchezaji mwenzake kufunga.
Kwa upande mwingine, wachezaji kama Stephane Aziz Ki wa Yanga, Josephat Bada na Ande Koffi wa Singida Black Stars, Yacouba Songne na Heritier Makambo wa Tabora United, pamoja na Salehe Masudi wa Pamba na Ismail Mgunda wa Mashujaa, wanashika nafasi ya tatu kwa kutoa asisti tatu kila mmoja. Hii inaonesha ushindani mkubwa katika ulingo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo kila mchezaji anahitaji kujiimarisha ili kuendelea kuwa kwenye orodha ya wachezaji bora.
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply