Yanga SC Yaondoka na Wachezaji 25 Kwenda Algeria Kuivaa MC Alger

kikosi cha yanga kilichoenda Algeria

Yanga SC Yaondoka na Wachezaji 25 Kwenda Algeria Kuivaa MC Alger

Kikosi cha Yanga SC chenye wachezaji 25, kimeondoka Dar es Salaam jana mchana, Desemba 3, 2024, kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo muhimu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya MC Alger.

Mchezo huu, unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa 5 July 1962 katika mji mkuu wa Algiers, ni wa pili kwa Yanga kwenye hatua ya makundi Kundi A, na umepangwa kufanyika Jumamosi, Desemba 7, 2024, saa 4 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Yanga SC inaingia kwenye mchezo huu ikitafuta matokeo mazuri baada ya kupoteza mchezo wa kwanza nyumbani kwa mabao 2-0 dhidi ya Al Hilal. Ili kuongeza matumaini ya kusonga mbele, benchi la ufundi limehakikisha kuchagua kikosi bora kilichojumuisha wachezaji wenye uzoefu na vijana wenye ari kubwa.

Yanga SC Yaondoka na Wachezaji 25 Kwenda Algeria Kuivaa MC Alger

Wachezaji wa Yanga Sc walio safiriri kuelekea Algeria:

Makipa

  • Djigui Diarra
  • Aboutwalib Mshery
  • Khomein Abubakar

Mabeki

  • Bakari Mwamnyeto
  • Dickson Job
  • Ibrahim Abdullah ‘Bacca’
  • Kouassi Yao Attohoula
  • Nickson Kibabage
  • Kibwana Shomari
  • Chadrack Boka

Viungo

  • Maxi Nzengeli
  • Pacome Zouzoua
  • Mudathir Yahya
  • Khalid Aucho
  • Stephane Aziz Ki
  • Denis Nkane
  • Sheikhan Khamis
  • Duke Abuya
  • Clatous Chama
  • Jonas Mkude
  • Farid Mussa

Washambuliaji

  • Kennedy Musonda
  • Clement Mzize
  • Prince Dube
  • Jean Baleke

Kuelekea mchezo wa pili wa makundi ligi ya mabingwa Yanga SC inakabiliana na changamoto ya kurejesha morali baada ya kupoteza mchezo wa awali, huku MC Alger wakitoka sare ya 0-0 dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wao wa kwanza. Ushindi wa MC Alger ugenini utawapa nafasi ya kujiimarisha kileleni mwa Kundi A, hivyo Yanga itahitaji kucheza kwa nidhamu na mbinu madhubuti kuwakabili wapinzani wao.

Uwanja wa 5 July 1962 unatarajiwa kuwa na presha ya mashabiki wa MC Alger, lakini Yanga SC inajivunia uzoefu wa wachezaji kama Stephane Aziz Ki, Clatous Chama, na Kennedy Musonda ambao wamekuwa muhimu katika mechi za kimataifa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Chikola wa Tabora United Akwepa Vita ya Ufungaji Bora
  2. Mshambuliaji wa Zamani wa Yanga Ajiunga na ZESCO Ndola Girls
  3. Kocha Taoussi Aweka Mtego Kuingilia Utawala wa Simba na Yanga
  4. JKT Tanzania Yatamba Kuendeleza Vichapo Ligi Kuu
  5. Yanga Yaibuka na Ushindi wa 2-0 Dhidi ya Namungo
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo