Matokeo ya Yanga vs Namungo leo 30/11/2024

Matokeo ya Yanga vs Namungo leo 30 11 2024

Matokeo ya Yanga vs Namungo leo 30/11/2024 | Matokeo ya Yanga leo Dhidi ya Namungo 31 Novemba 2024

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, leo wanatarajiwa kushuka dimbani kuwakabili Namungo FC katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya msimu wa 2024/2025. Mchezo huu utachezwa kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, Mkoani Lindi, huku kila timu ikiingia kwenye mchezo huu ikiwa na malengo ya kupata matokeo bora, baada ya kutoweza kuvuna pointi katika mechi zao za hivi karibuni.

Namungo, ambayo imekuwa na mwenendo usio ridhisha kwenye ligi msimu huu, imepoteza mechi nane kati ya 11 ilizocheza. Hali hii inawafanya kuingia kwenye mchezo huu wakiwa na presha ya kupata ushindi muhimu ili kupanda katika msimamo wa ligi. Kwa sasa, Namungo inashika nafasi ya 13, ikiwa na pointi tisa kutoka kwenye michezo 11 ilizocheza.

Kwa upande mwingine, Yanga SC, ambao walikuwa na mwendelezo mzuri mwanzoni mwa msimu, wamepoteza mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu dhidi ya Azam FC na Tabora United. Yanga, ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu, wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na pointi 24 na wanahitaji ushindi ili kupunguza pengo la pointi na watani wao wa jadi, Simba SC, ambao wanashika nafasi ya kwanza kwa sasa wakiwa na pointi 28.

Matokeo ya Yanga vs Namungo leo 30/11/2024

Namungo 0-2 Yanga SC
  • Dakika ya 85โ€ฒ Assist Chamaโ€ฆ.Goli Pacome; Goli la pili kwa Yanga.
  • Goooooalโ€ฆ..!!! Kennedy Musonda dakika ya 50.
  • ๐Ÿšจ#๐Œ๐€๐“๐‚๐‡๐ƒ๐€๐˜๐๐๐‚๐๐‹ ๐Ÿšจ
  • Namungo Fc ๐Ÿ†š๏ธ Yanga Sc
  • ๐Ÿ† NBC Premier league
  • ๐Ÿ—“ 30/11/2024
  • โฑ ๐’๐š๐š ๐Ÿ๐Ÿ:๐Ÿ‘๐ŸŽ ๐‰๐ข๐จ๐ง๐ข
  • ๐ŸŸ๏ธ ๐”๐ฐ๐š๐ง๐ฃ๐š ๐ฐ๐š ๐Œ๐š๐ฃ๐š๐ฅ๐ข๐ฐ๐š, ๐‘๐ฎ๐š๐ง๐ ๐ฐ๐š ๐‹๐ข๐ง๐๐ข

Matokeo ya Yanga vs Namungo leo 30/11/2024

Yanga SC inashuka uwanjani leo baada ya kupoteza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal, mchezo uliochezwa Novemba 26, 2024, na kumalizika kwa matokeo ya 2-0 kwa faida ya wageni. Kipigo hiki kilikuwa cha pili mfululizo kwa Yanga, wakiwa wamepoteza mechi mbili za Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Kwa hivyo, kocha mpya wa Yanga, Sead Ramovic, atakuwa akiongoza timu yake kwenye mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu baada ya kuchukua mikoba kutoka kwa Miguel Gamondi. Ramovic anahitaji ushindi ili kuhakikisha timu yake inarejea kwenye ushindani wa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu.

Namungo, licha ya kushuka kwao kwenye msimamo wa ligi, pia wanahitaji matokeo mazuri ili kuondokana na hali mbaya ya matokeo. Kocha Juma Mgunda, ambaye alichukua mikoba ya Mwinyi Zahera kama kocha mkuu wa Namungo, ana malengo ya kuleta mabadiliko ya haraka ili kurejesha morali ya wachezaji na kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi.

Historia ya Mkutano wa Timu Hizi

Katika historia ya mechi kumi zilizopita za Ligi Kuu kati ya Yanga na Namungo, Yanga SC inaonekana kuwa na wigo mkubwa wa ushindi. Yanga imeshinda mechi tano, huku Namungo ikiwa haijawahi kupata ushindi. Yanga imeshinda mechi mbili ugenini na tatu nyumbani, na pia imepata sare mbili ikiwa nyumbani na tatu ikiwa ugenini. Kwa upande wa mabao, Yanga imeifunga Namungo mabao 15, huku Namungo ikifunga mabao saba tu kwa Yanga katika mechi hizo kumi.

Kwa hivyo, Namungo itahitaji kuwa na utayari wa kipevu ili kuvunja mwiko wa kutoshinda dhidi ya Yanga, huku Yanga ikitarajia kurejea kwenye ushindi baada ya kipigo cha karibuni.

Mapendekezo ya Mhariri;

  1. Kikosi cha Yanga vs Namungo leo 30/11/2024
  2. Yanga vs Namungo leo 30/11/2024 Saa Ngapi?
  3. Tabora United Yaendelea Kugawa Dozi Ligi kuu
  4. Sandaland Yamtaka Ally Kamwe Kulipa Billion 3 Ndani Ya Siku 7
  5. Camara Aonya Kuhusu Ugumu wa Michuano ya CAF
  6. Simba na Yanga Zaekwa Kiporo Ratiba Mpya ya Kombe la FA
  7. Yanga Yapania Kurejea Kwa Kasi ya kimbunga Ligi Kuu
  8. Luhende Aonya Mastaa wa Soka Kuhusu Starehe Kupita Kiasi
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo