Tabora United Yaendelea Kugawa Dozi Ligi Kuu
Klabu ya Tabora United imeendeleza kiwango bora walichonacho kwa sasa kwenye Ligi Kuu NBC baada ya kushinda mchezo wao dhidi ya Kinondoni Municipal Council F.C. (KMC) kwa goli 2-0. Magoli ya Yacouba Sogne ’43 na Offen Chikola ’59 yalitosha kupeleka alama 3 kwa warina asali hao wa tabora ikiwa ni mchezo wao wa nne mfululizo kushinda.
Baada ya ushindi huu, sasa wamepanda mpaka nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara 2024/2025 wakijikusanyia alama 21 huku Kocha mpya wa KMC Kali Ongala akianza vibaya kibarua chake kwa wakusanya ushuru hao kutoka Manispaa ya Kinondoni.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Sandaland Yamtaka Ally Kamwe Kulipa Billion 3 Ndani Ya Siku 7
- Camara Aonya Kuhusu Ugumu wa Michuano ya CAF
- Simba na Yanga Zaekwa Kiporo Ratiba Mpya ya Kombe la FA
- Yanga Yapania Kurejea Kwa Kasi ya kimbunga Ligi Kuu
- Luhende Aonya Mastaa wa Soka Kuhusu Starehe Kupita Kiasi
- Mapambano Makali Yanaendelea Championship 2024/2025
- Tanzania Yapanda kwa kasi katika Viwango vya FIFA
Leave a Reply