Zamalek Yashinda Kombe la Shirikisho CAF 2023/2024

Zamalek Yashinda Kombe la Shirikisho CAF 2023/2024 | Mshindi wa Kombe la shirikisho CAF

Jiji la Cairo liligeuka kuwa bahari ya shangwe na furaha usiku wa kuamkia Jumatatu, huku maelfu ya mashabiki wa klabu ya Zamalek wakiujaza Uwanja wa Kimataifa wa Cairo kusherehekea ushindi wa kihistoria wa klabu yao.

Ushindi huu ni wa pili kwa Zamalek katika historia ya Kombe la Shirikisho, wakiwa walitwaa taji hilo kwa mara ya kwanza mwaka 2019, pia dhidi ya RS Berkane. Ni wazi kwamba ushindi huu una maana kubwa kwa klabu, mashabiki, na taifa zima la Misri.

Zamalek Yashinda Kombe la Shirikisho CAF 2023/2024

Zamalek Yashinda Kombe la Shirikisho CAF 2023/2024

Zamalek, maarufu kama “The White Knights,” wameibuka Mabingwa wapya wa Kombe la Shirikisho la CAF 2023/2024 baada ya kuishinda RS Berkane ya Morocco kwa jumla ya mabao 2-2, huku bao la ugenini likitumika kama kigezo cha kumpata bingwa.

Mchezo wa marudiano wa fainali ya CAF confederation cup almaharufu kama kombe la shirikisho Afrika, ulikuwa ni mtanange wa kipekee, uliojaa mbinu, ufundi, na mchezo wa kusisimua. Zamalek, wakiwa wamepoteza mchezo wa kwanza nchini Morocco kwa mabao 2-1, walijua walichotakiwa kufanya ili kutwaa taji hilo. Na walifanya hivyo kwa mtindo wa kipekee baada ya kushinda mechi ya marudiano kwa goli 1-0.

Kiungo mshambuliaji machachari, Ahmed Hamdi, aliibuka shujaa wa usiku huo. Bao lake la dakika ya 23, lililotokana na pasi maridadi ya Ahmed “Zizo” Sayed, liliipa Zamalek bao muhimu na kusawazisha matokeo kwa jumla. Bao hilo liliamsha shangwe zisizo kifani uwanjani, huku mashabiki wakishangilia kwa nguvu, wakipeperusha bendera na kuimba nyimbo za ushindi.

Mchezo huo ulikuwa ni mtihani mkubwa kwa Zamalek, kwani RS Berkane walipambana vikali kutafuta bao la ugenini ambalo lingewapa ushindi. Hata hivyo, safu ya ulinzi ya Zamalek, chini ya uongozi wa kipa Mohamed Awad, ilionyesha nidhamu ya hali ya juu na kuzuia mashambulizi yote ya Berkane.

Zamalek walicheza kwa nidhamu, wakipiga pasi fupi fupi na kuwakabili wapinzani kwa nguvu. Walifanikiwa kudhibiti mpira na kuzuia Berkane wasiweze kuunda nafasi za wazi za kufunga. Hata baada ya Hamdi kutoka nje kwa jeraha, Zamalek waliendelea kucheza kwa kujiamini na kudhibiti mchezo.

Mapendekezo Ya Mhariri:

  1. Historia Mpya Yaandikwa: Man City Yanyakua Taji la EPL kwa Mara ya 4 Mfululizo
  2. Marefa wa Tanzania waliochaguliwa Kuchezesha Michezo ya Kufuzu Kombe la Dunia
  3. Timu Zilizofuzu UEFA Champions League 2024/2025
  4. Magoli Mawili ya Haaland Yarejesha Man City Kileleni mwa Msimamo wa Ligi
  5. Mvua Yafichua Ubovu wa Old Trafford: Video ya Kuvuja Maji Yatisha Mashabiki
  6. Yanga SC Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania 2023/24: Ushindi wa Mara ya 30 Kihistoria
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo